Chuki Ya Nini?

Chuki Ya Nini?

Gily Gru

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2016
Posts
8,632
Reaction score
23,673
Siku hizi kila unapoenda iwe kitaa, ofisini au kwenye mitandao ya kijamii watu wanaleta chuki bila sababu ya msingi. Watu wakikuona una maendeleo binafsi na unavaa unapendeza wanakushambulia kwa maneno ya fitina au majungu tu ili kukukatisha tamaa. Wengine wanadiriki kabisa kukushambulia Mungu alivyokuumba kana kwamba wewe umejiumba mwenyewe vile. .

Mimi binafsi nimezaliwa mweupe na Mungu kaniumba hivyo mweupe peeee sasa sijui kwa nini watu wanakerwa sana na mimi kuwa mweupe kana kwamba ni kitu ambacho nimekichagua. Mungu kapanga niwe kijana mwanaume mweupe pee sasa watu wanaloga, wengine wanasema maneno machafu: eti mweupe kama papai, mara mweupe mpaka unakera, mara ungekuwa albino, wengine wananiita albino shida sana ila kuna watu wanakera sana wanavuka mipaka wananiita cheupe badala ya kuiniita white, ili tu waniuzi sijui wanapata faida gani.

Nimegundua kitu kimoja baada ya kuona atu wananishambulia wakati sijwahi hata kupoteza mda wao. Nimegundua watu wafupi wanachukia sana watu warefu wakati watu warefu hawana mda kuhangaika kuwashambulia wafupi. Watu weusi tiii huwa wanashambulia sana watu weupe huku watu weupe hawana shida ya kuwashambulia watu weusi. Kuna watu wanashambulia sana watu wembamba kisa tu wao ni vibonge wanawaonea wivu kwa sababu tu zao binafsi.

Ukiona mtu anakushambulia jinsi Mungu alivyokuumba kaa nao mbali hao watu ni wale wale wenye chuki hawawezi na hawatoweza kuwa wa maana katika maisha yako. Furahi sana jinsi Mungu alivyokuumba kwani amekuumba kwa mfano na sura yake mwenyewe. Acheni kujichubua, kujikondesha, kujiongeza viungo au kupunguza makalio kwa sababu ni kufuru kwa Muumba wa nchi na mbingu. .
 
Sambaza upendo kwa kusema neno “One Love”. .

Ningezaliwa mweupe ningejipaka ata oil chafu kabisa.

Mimi siwezi Mpangia Mungu kwa kuniumba mweupe naamini hata mwenyewe Mungu ni Mweupe kama kaniumba kwa sura na mfano wake yeye. .

Wewe sambaza chuki tu unampangia hadi aliyekuumba ila si umesema wasambaza chuki usiku wanalala mda ukifika utalala tu au sio?
 
Mim sijasema nachuki
Mim nafagilia weusi wangu tu. Ulitaka niseme nataman kuwa mweupe?
 
Mim sijasema nachuki
Mim nafagilia weusi wangu tu. Ulitaka niseme nataman kuwa mweupe?

Wewe umesema ungekuwa mweupe ungepaka hata oil, ina maana unachukia weupe
Mbona mie sichukii weusi yote sawa tu

Ila kwenye scale ya 1 mpaka 10 weusi wako unaweza kuwa namba ngapi??
 
Wewe umesema ungekuwa mweupe ungepaka hata oil, ina maana unachukia weupe
Mbona mie sichukii weusi yote sawa tu

Ila kwenye scale ya 1 mpaka 10 weusi wako unaweza kuwa namba ngapi??
Kila mtu afagilie cha kwake full stop.
 
Kila mtu afagilie cha kwake full stop.

Huna chako sijui unafagilia nini
Ulaya huko watu wanajisifu kwa kuwa na mali za fahari huku bongo watu wanajisifu rangi ya mwili haha
 
Piga kazi watakuchukia maana imenenwa ila watakubali tu

Sent using Jamii Forums mobile app

Maneno huwa yanachoma kama kisu wengine wanatumia maneno kuzungumza, kuwapatanisha, kuwakutanisha, kusambaza upendo nk huku wengine hutumia kama silaha kuleta, chuki, fitina na majungu. .
 
Huna chako sijui unafagilia nini
Ulaya huko watu wanajisifu kwa kuwa na mali za fahari huku bongo watu wanajisifu rangi ya mwili haha
Tupo ulaya Tena???

Cheupe punguza attitude.
 
Nikweli Man.... Awali hata Mimi nilikua najitahidi kua MTU wawatu, nawakopesha n.k

Maajabu wale naowakopesha, wanashindwa kunirudishia, na ndo kwanza wananichukia bila sababu.

Saizi sina mpango wakumkopesha mtu
 
Mimi ni kibonge, mweusi, mfupi, kithembe alafu sina hela ila fresh tu. Najiiamini balaa, nabishana mpaka kesho. Jiamini asee!
 
Mie nimekopesha watu wengi si kwa sababu ninazo ila tu kwa sababu nao wanyanyuke maana wako pabovu kushinda mimi. Kuna mtu hajibu message wala hapokei simu, watu wa ajabu sana. .

Mwaka huu nimeanza na sera sikopeshi kabisa sitaki urafiki kwenye hela kama alikuwa na mpango wa kunichukia anichukie tu. Kuna mmoja nilimuliza kwani aliyekuambia mie nina hela nani au unatafuta sababu gu? lile lijamaa halielewi kabisa
 
Mimi ni kibonge, mweusi, mfupi, kithembe alafu sina hela ila fresh tu. Najiiamini balaa, nabishana mpaka kesho. Jiamini asee!

Tatizo sio kujiamini mbona mie najiamini kwa kila nachokifanya. Nimesema watu wanaleta chuki sana ili kuwakwamisha wenzao na wengine wanashambulia jinsi Mungu alivyokuumba

Haimanishi kwa kuwa wewe ni kibonge, mfupi, mweusi basi ni wale wale mbona kama unajiamini Mr -KANA- umejishtukia kama nakusema wewe?

Sijamaanisha kwa kuwa mtu ni mfupi, au mweusi au kibonge basi ana chuki nisamehe bure
 
Back
Top Bottom