Chuki yangu na trafiki imegoma kuondoka

Chuki yangu na trafiki imegoma kuondoka

Hawa watu huwa wanakufa vifo vibaya sana kutokana na dhulma zao, kwanza hawana utu kabisa mola awalaaani na makaburi yao yawe mashimo ya choo motoni.
Kifo kibaya kimemkuta mmoja wao majuzi tu hapo Mang'ula ilikuwa hivi; jamaa (trafiki) kamaliza kukagua gari (Fuso) akawa anaandaa mkeka huku kasimama pembeni ya cabin, aisee ghafla bin vuu ilitokea boda kwa speed kali sana ikapita nae akaenda chini kapigiza sehemu ya nyuma ya kichwa.

Alivuja damu ya kutosha kumuwahisha hospitali akakatia moto njiani, ikawa Bwana ametoa bwana ametwaa....

Manung'uniko yakizidi hugeuka laana, asanteni sana. Nikiripoti toka pande hizi mimi ni KB wa JF.
 
Watu hawa wana tamaa na roho mbaya iliyopitiliza

Sent from my SM-A025F using JamiiForums mobile app
Wana roho mbaya sana kima wale, mwezi August natoka Dar nimefika maeneo ya kibaha kwa Matias mbele mbele kidogo kuna kama kimteremko cha mchongo. Mbele yangu kulikuwa na lorry nikacheki usalama nikaona fresh ngoja nilipite lorry!!! Mweee kumbe kuna haya makima yamejificha mahali kwenye mwinuko.

Kanipiga mkono nikaweka kushoto, sikushuka akaja mlangoni naomba leseni yako nikampa, naomba kadi ya gari nikampa, naomba sticker ya week ya nenda kwa usalama nikamwambia cheki pale nyuma. Mara akaanza hii gari umekata bima? Nikamwambia ndio nimekata kama vipi cheki kwenye Tiramis.

Huyu dada ni mjinga na mpumbavu shenzy kabisa, ujue nini...akabadilisha subject toka kwenye kukagua gari kwenda kwenye kosa la ku-overtake sehemu isiyoruhusiwa tukavutana pale mie nakomaa kuwa pale ni mahali sahihi hakukua na double barrier nilizingatia hilo kabla sijaovertake kazidi kukomaa tu, mwisho kabisa nikamwambia unatakaje? Moyoni najua anachokitaka, akajibu nakuandikia faini.

Nikaona ananipotezea muda nikafungua mahali nikatoa afutano nampa eti anajitia kukataa anataka zaid. Aisee alinivuruga nikamwambia Oya sister isiwe shida andika hiyo faini huku natia gear, kuona sina habari nae akasema nipe hiyo hiyo usirudie tena. Ilibidi nicheke tu nikaondoka zangu. Hawa ni washenzi na wanatembea na laana za wengi kima kabisa wale
 
Kifo kibaya kimemkuta mmoja wao majuzi tu hapo Mang'ula ilikuwa hivi; jamaa (trafiki) kamaliza kukagua gari (Fuso) akawa anaandaa mkeka huku kasimama pembeni ya cabin, aisee ghafla bin vuu ilitokea boda kwa speed kali sana ikapita nae akaenda chini kapigiza sehemu ya nyuma ya kichwa.

Alivuja damu ya kutosha kumuwahisha hospitali akakatia moto njiani, ikawa Bwana ametoa bwana ametwaa....

Manung'uniko yakizidi hugeuka laana, asanteni sana. Nikiripoti toka pande hizi mimi ni KB wa JF.
Acha kutufunga kamba za vijiwe vya bodaboda

Sent from my SM-A217F using JamiiForums mobile app
 
Katika watu ambao wanaleta kero kwa madereva barabarani ni traffic yani wako kwa ajili ya kupata ela za kuminyiwa au kupiga fine.
 
Juzi kait nilikamatwa, nilipita na red. akajifanya anabonyeza dizain kama anataka kutoa mkeka, nikauchuna tu, baadae akaniuliza vipi nikuandikie faini au utanipa ya chai? nikazama mfukoni nikamtolea buku tano. sasa kuna afsa mwenzake anakodolea nikasita kidogo, avyoona nimesita akaniambia we weka chini yaleseni ama kadi ya gari.
Nikatoa ile hela na tabasamu juu usoni ila moyoni inaniuma.
 
Back
Top Bottom