Chuki zingine za kujitakia - Watumishi wa Umma hawatapigia kura kamwe CCM 2020

Chuki zingine za kujitakia - Watumishi wa Umma hawatapigia kura kamwe CCM 2020

Mkuu Tila Lila, wakati hoja zako ni mgombea atakayeahidi..., by Octoba mwakani, mgombea wa CCM sio anapanda jukwaani kuahidi, bali kuelezea utekelezaji wa yote hayo na mengine kibao, hivyo kura zote za watumishi wa umma kwa uchaguzi mkuu wa 2020 ni kwa CCM!.
Kununi itakayotumika kuhakikisha kura hizi ni kwa CCM ni ile kanuni ya "penye udhia..."

P

Mkuu watumishi wa umma kwa sasa wana muamko na wanajitambua tofauti kabisa na ilivyokua hapo awali. Wale watiifu wengi wa ccm wameshastaafu. Hivyo hata watudaganyie kwa kuongeza hela kiduchu kwenye mishahara, wapandishe madaraja, nk. Bado Ccm ingeangushwa tu maana imechokwa na Watanzania tulio wengi.

Kinachoibeba hiyo Ccm na wagombea wake siku zote ni kutokuwepo tu kwa Tume inayoeleweka ya uchaguzi, Kuwapa jukumu makada mfano Wakurugenzi, Ma Dc, Ma Rc, nk. kusimamia zoezi la uchaguzi, polisi kutumika vibaya, nk.

Kungekua na Demokrasia ya kweli nchini, Ccm ingekua imeshajifia kitambo tu. Kwa sasa ina lazimisha kupendwa! Ila kimsingi imeshachokwa. Watanzania wengi tunataka mabadiliko.

Hivyo watumishi wengi tunaojitambua, hatutoshiriki kwenye maigizo yoyote yale yanayoitwa uchaguzi! Maana tunafahamu mshindi atakua nani! Sasa ya nini kupoteza muda? Hasa katika awamu hii ya tano! Labda itokee hatua za msingi zikachukuliwa kupunguza haya madhaifu yaliyopo, tutarudisha imani.
 
Mkuu Tate, kwanza naunga mkono hoja zako ikiwemo ya
Watanzania wengi tunataka mabadiliko, lakini hayo mabadiliko alete nani?.
Kumbe mmeishafahamu uchaguzi ni maigizo, mshindi anajulikana, kwanini tusiufute tuu kabisa uchaguzi na Magufuli aendelee tuu?.
P
 
Mnataka Aongeze Mshahara gharama za Maisha zipande?

Sent using Jamii Forums mobile app
[/QUOT
Mkuu Tila Lila, wakati hoja zako ni mgombea atakayeahidi..., by Octoba mwakani, mgombea wa CCM sio anapanda jukwaani kuahidi, bali kuelezea utekelezaji wa yote hayo na mengine kibao, hivyo kura zote za watumishi wa umma kwa uchaguzi mkuu wa 2020 ni kwa CCM!.
Kununi itakayotumika kuhakikisha kura hizi ni kwa CCM ni ile kanuni ya "penye udhia..."

P
Hili halipo hata Kama atapandisha mshahara Mara mbili
 
Ndg tupiganie tume huru ya uchaguzi, vinginevyo itakuwa kama serikari mitaa.
Akili itawarudi nyote watumishi, wakulima na wafanya biashara.
Bila kuwa na tume huru ya uchaguzi, hakuna uchaguzi wa haki!!
 
Kazi hamfanyi kutwa kudai mishahara
Mshahara ni huo huo kilichokatwa ni hela ya wizi hakuna,chupi zinawabana
Dawa ni kuacha kazi tu,badala ya kutishia kunyima ccm kura
Hivi kwa akili yako watumishi wote wa serikali msipigie kura ccm ndio itaondoka madarakani?
 
Mkuu mtu wa idara gani hatampigia kura Magufuri au CCM 2020 kwa sababu ya kutopata increment au nyongeza ya mshahara???
Hujui kama wengi waliosaidia kuhujumu zoezi la uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 ni watumishi wa umma??

Hujui hata polisiem pia wanatumika lakini vimishahara vyao ni hivi vya tunakutakia ufe mapema iwezekanavyo!
 
Yani upewe kitambulisho cha NIDA na fingerprint, usajili simu yako na fingerprint, kitambulisho cha kupigia kura na fingerprint, HALAFU usimpigie kura?!

Kwanza kura zenu zimeshapigwa, nyie hata msijisumbue taarifa zenu ziliisha ingizwa kwenye mfumo wa BVR na kura mliisha mpigia Magufuli.

Nendeni mkasajiri simu zenu zoezi liwe rahisi zaidi, sasa wanahitajika wale wa vijijini, msio kuwa na simu, vitambulisho nyie msijisumbue nyie siyo watanzania hivyo Kira hamtopiga.
 
Back
Top Bottom