SoC02 Chukua tano zangu za dhahabu na mtaji wako utafanikiwa

SoC02 Chukua tano zangu za dhahabu na mtaji wako utafanikiwa

Stories of Change - 2022 Competition

MKAKA WA CHUO

Member
Joined
Aug 13, 2022
Posts
11
Reaction score
6
Utajiri: Ni Hali ya MTU au watu kujitosheleza Katika nyanja tofautitofauti za kiuchumi. Utajiri unaweza kuhusisha vitu Kama vile mifugo, mashamba, mali au pesa. MTU huitwa tajiri kwa kumiliki vitu Kama vile mashamba makubwa yanayompatia faida, maduka makubwa, magari, majumba,migodi na vitu vingine vinavyoweza kumuingizia kipato kikubwa.

Katika hali ya kawaida utajiri ni miongono mwa malengo ya vijana walio wengi ingawaje kunachangamoto mbalimbali zinazowakabili vijana na WATANZANIA kwa ujumla katika kufanikisha kuupata utajiri huo utukanao na jasho lakila mmoja wao binafsi. Kutokana na SABABU mbalimbali, utajiri umekuwa ni KITUO Cha mbali mno kufikiwa na WATANZANIA walio wengi husasani vijana.

Kiuhalisia kuwa tajiri sio jambo rahisi kwasababu, ili MTU kuwa tajiri inamuhitaji MTU awe mvumilivu,mbunifu, mwenye kujitoa na kufanya kazi bila ya kukata tamaa, hivyo ukiangalia vitu vyote hivyo vinahitaji MTU mwenye msimamo na matarajio ya kufikia Lengo Hilo la utajiri. Kama kijana au mtanzania yeyote kuna njia au namna mbalimbali ambazo zinaweza kukusaidia kufikia Lengo lako la utajiri, zifuatazo ni miongoni mwa njia zitakazo kukusaidia kufikia Lengo la utajiri:


Kwanza; Kama kijana hakikisha unakuwa na malengo yako binafsi na unayasimamia na kuyapambania. Malengo ndio msingi mkuu unaongoza shughuli yeyote kabla ya kuanza kwa shughuli hiyo, kukosekana kwa malengo katika shughuli za vijana wengi kumepelekea wengi katika vijana kujihusisha katika shughuli zinazowapatia kiwango kidogo Cha fedha kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya chakula na vocha jambo ambalo sio la sawa kwa mtizamo wa jicho la pili, hii ni kwasababu Kama kijana wewe Nini baba au mama matarijiwa Sasa vipi utaendesha familiya yako Kama haukuweka malengo ya kuyafikia yakiwa Kama mafanikio.


Pili; Kama kijana hakikisha suala la kujali muda katika harakati zako za maisha zinazokuingizia kipato. Kwa mfano wewe ni mkulima basi hakikisha unaandaa shamba kabla Mvua za kupanda hazijanyesha, au bodaboda lazima ujue muda gani uamke kwa SABABU muda huo ndio ambao watu wengi wanahitaji usafiri ili kuelekea sehemu tofautitofauti Kama vile kazini, stendi za mabasi, treni na bandarini ,lakini kitendo Cha dereva wa bodaboda kuamka saa tatu hii inachangia katika kurudisha nyuma ndoto ya mafanikio katika safari yetu hii ya maisha, kwasababu muda ni rasilimali pekee ambayo ikiipoteza hautoweza kuifidia daima.


Tatu; Kama kijana lazima ujue kutofautishwa kati ya kipato unachopata na matumizi unayotakiwa kufanya, Hali ya kutokuzingatia matumizi, imepelekea vijana wengi kufanya kazi kwa muda mrefu pasi na kupata tija inayolingana na wakati na nguvu walizotumia, kwa mfano dereva wa bodaboda anaingiza elfu thelathini kwa siku, katika pesa hiyo bosi atampa tuseme elfu 10, saa nne Asubuhi atakunywa chai ya maziwa ya miatano, chapati tatu za elfu moja na miatano, na supu ya elfu moja na miatano, jumla kwa Asubuhi tu kijana huyu wa bodaboda ametumia shilingi elfu tatu na miatano. Ikifika saa Tisa na nusu jioni ataenda Tena mgahawani atakula sahani moja ya wali nyama ambayo ni elfu mbili na soda moja ya miatano, jumla atatumia elfu mbili na miatano kwa mchana hapo bado Usiku tufanye atatumia elfu mbili na atanunua vocha ya elfu moja na pesa itakayo bakia ni ya mafuta. Kijana unatakiwa ukumbuke huyo aliyekupa wewe hiyo bodaboda alikuwa anakula miogo ya mia tano na chai ya miambili wakati yeye alipokuwa na malengo ya kumiliki pikipiki na alipokuwa na pikipiki mbili, moja alimpa kijana Kama hivyo wewe na nyingine alikuwa akiendesha yeye mwenye Kama dereva wa bodaboda, vijana wengi wana matumizi makubwa ukilinganisha na vipato vyao, vijana tupambane kwanza tukifanikiwa tutatumia, Kumbuka hakuna tajiri asiyekuwa na bajeti katika matumizi yake hata ukipata pesa nyingi bila kuwa na bajeti utafilisika.


Nne; Kama kijana hakikisha unaishi na watu vizuri na ujihakikishie uhusiano mzuri na watu muhimu. Kitendo Cha vijana wengi kujitenga na watu katika jamii kinasababisha ugumu katika nyakati mbalimbali, kwa mfano suala la ajira za muda za sensa, Kama kijana unaeleweka na viongozi wakata yako na walimu wa shule za maeneo yenu utakuwa na uwezekano mkubwa wewe Kama kijana kupata nafasi hii, lakini kwasababu vijana wengi wenye shahada na stashada zao wamejitenga mitaani bila kutafuta watu wenye cheni za maisha, wengi wao katika vijana hao wanaendelea kulalamika maisha magumu, Kama kijana hakikisha unakuwa na uhusiano mzuri na watu wenye cheni za mafanikio katika maisha bila ya kujali umri, jinsia Wala dini zao, siku hizi mafanikio huja kwa cheni. Hivyo vijana tuishi na watu vizuri, dharau, kejeli na majivuno kwa SABABU ya shahada zetu zinaweza kutuchelewesha, maisha ni watu na watu ndio cheni, basi TUISHI na watu vizuri.


Tano; Kama kijana ili ufanikiwe, lazima uepukana na makundi ya ovyo, uepuke kuiga vitu visivyo na msingi, ujitoe na Umuamini MUNGU wako. Suala la makundi ya ovyo Kama vile walevi, wavuta bangi na wabugiaji wa unga ni miongoni mwa changamoto inayochangia udumavu na ukosefu wa mawazo mapya na chanya kwa vijana wengi wanaojihusisha na makundi Haya, Kama kijana wa kitanzania ili uweze kupiga hatua katika maisha yako lazima uepukane na makundi hayo machafu. Jambo la kuiga hususani kwa wadada, wengi katika wadada ikiwemo wanachuo na wengineo, wanapenda kuiga maisha ya wasanii wakati hao wasanii wameshapiga hatua tayari. Kwa mfano msichana anayefanya kazi mgahawani au mwanachuo anamlipa msusi elfu thelathini Kila baada ya siku ishirini au mwezi, wakati misuko ya Bei ndogo ipo, Hali hii ndio inapelekea wadada wengi kuchelewa kupiga hatua. Vilevile kujitoa, vijana wengi wakitanzania bado tuna fikra hasi katika kujaribu miradi tofauti tofauti kwa mfano kilimo Cha KISASA, biashara na miradi mingine, Kama kijana lazima ujue kwamba bila ya kujitoa na kusimamia kikamilifu mradi hautoweza kuwa tajiri daima, hivyo vijana lazima tujutoe na tuthubutu na hatimaye tutafanikiwa.

Lakini jambo jingine la msingi ni kumuani MUNGU Wako, Kama mtanzania hakikisha unamuamini mungu wako katika hali na shughuli zote ziwe nyepesi au nzito unazozipitia katika maisha Haya ya Kila siku, kitendo Cha kutokumuamini MUNGU siku hizi kumepelekea vijana wengi kumaliza muda na fedha nyingi kwa waganga wa kienyeji bila ya kupata mafanikio yoyote, Kama kijana au Kama mtanzania ongeza juhudi kazini, ondoa vyanzo vya changamoto kazini, kuwa mvumilivu hatimaye utaitwa tajiri na sio kukesha kwa waganga wa kienyeji kwasababu huko kutakupotezea muda na fedha nyingi. Hapo chini ni picha kutoka katika akaunti ya twitter ya bilionea kijana wa kitanzania MOH DEWJI akihamasisha jamii juu ya kujali muda,kumuamini mungu na kutokata tamaa na kuwajibika.

NDUGU ZANGU WATANZANIA, UTAJIRI NI MTAMU SANA, UNAHITAJI JITIHADA SANA, TUKAZE BUTI.

BY MKAKA WA CHUO.
 

Attachments

  • Screenshot_20220815-045102.png
    Screenshot_20220815-045102.png
    8.2 KB · Views: 58
  • Screenshot_20220815-045055.png
    Screenshot_20220815-045055.png
    10.2 KB · Views: 56
  • Screenshot_20220815-045035.png
    Screenshot_20220815-045035.png
    135.3 KB · Views: 56
  • Screenshot_20220815-045009.png
    Screenshot_20220815-045009.png
    10.5 KB · Views: 50
  • Screenshot_20220815-045143.png
    Screenshot_20220815-045143.png
    107.6 KB · Views: 51
  • Screenshot_20220815-044957.png
    Screenshot_20220815-044957.png
    10.1 KB · Views: 48
  • Screenshot_20220815-044146.png
    Screenshot_20220815-044146.png
    7.7 KB · Views: 50
Upvote 0
Back
Top Bottom