Chuma Ulete: Ni kweli ipo? Ipi dawa ya kuidhibiti?

Kinga nzuri dhidi ya chuma ulete​




Je unaijua Chuma ulete...? Kwa kisukuma wanaita *BHUGINDU
Na je unafahamu kinga yake na zuio ili wasikuibie pesa, unga, au chochote ndani mwako....?

Dawa ya kukinga ni hii ukipata mkaa ulio dondoka njiani basi uchukue nenda kauweke kwenye kapu la pesa ukiwa pamoja na tunda lile la njano la ndulele unaviweka pamoja.
Ili huyo mwenye chuma ulete pia ili asiweze kuingia ndani kwako kukwiba unga, pesa na chochote kile basi pale mlangoni unapoingilia napo ning'iniza ndulele na huo mkaa ukiwa umeuweka pamoja au ufunge kwenye kitambaa cheusi kisha uning'inize kwa mlango wako hutokaa uone hata chuma ulete anayekuja kukwibia vitu dukani au nyumbani kwako akijaribu ataumbuka mchana kweupe
 
Hatari sana
 
Watu ni wajinga sana.... Sehemu ambapo wanalinda kwa bunduki na sheria...pesa ikipotea mtu anakatwa mshahara huwezi sikia chuma ulete....ila hizi biashaza za ujinga ndio tunaambiana habari za chuma ulete... amkeni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…