Chuma Ulete: Ni kweli ipo? Ipi dawa ya kuidhibiti?

Chuma Ulete: Ni kweli ipo? Ipi dawa ya kuidhibiti?

Kinga nzuri dhidi ya chuma ulete​

Kinga nzuri dhidi ya chuma ulete.jpg



Je unaijua Chuma ulete...? Kwa kisukuma wanaita *BHUGINDU
Na je unafahamu kinga yake na zuio ili wasikuibie pesa, unga, au chochote ndani mwako....?

Dawa ya kukinga ni hii ukipata mkaa ulio dondoka njiani basi uchukue nenda kauweke kwenye kapu la pesa ukiwa pamoja na tunda lile la njano la ndulele unaviweka pamoja.
Ili huyo mwenye chuma ulete pia ili asiweze kuingia ndani kwako kukwiba unga, pesa na chochote kile basi pale mlangoni unapoingilia napo ning'iniza ndulele na huo mkaa ukiwa umeuweka pamoja au ufunge kwenye kitambaa cheusi kisha uning'inize kwa mlango wako hutokaa uone hata chuma ulete anayekuja kukwibia vitu dukani au nyumbani kwako akijaribu ataumbuka mchana kweupe
 
Wana jamii ningepanda kujua maana halisi ya chuma ulete kwani zaidi najua mtu anaye weza kuchukua hasa pesa kwa ki mazingira ndio huita chuma ulete. kuna siku jamaa mmoja alinikuta nanunua bidhaa duka ni a kaja kwangu na kuniomba shilingi Mia moja . nilikuwa na kiasi cha shilingi kadhaa mkononi nikampa mia akaenda pembeni yangu kulikuwa na mama mmoja alikuwa akinitazama kwa jicho la ishara alipoondoka yule jamaa yule mama akasema usinge mpa kwani km angekuwa na shida basi angeomba buku au Mia 5. Hawa watu wa aina hii ni washilikina wanafanya CHUMA ULETE.
sijapata madhara yeyote sasa yapata wiki . Je hili tukio laweza kuwa ni la kishirikina? na lina kaa active kwa muda gani? ...
Hatari sana
 
Watu ni wajinga sana.... Sehemu ambapo wanalinda kwa bunduki na sheria...pesa ikipotea mtu anakatwa mshahara huwezi sikia chuma ulete....ila hizi biashaza za ujinga ndio tunaambiana habari za chuma ulete... amkeni
 
Back
Top Bottom