Chumaulete ni uchawi au kiini macho?

Chumaulete ni uchawi au kiini macho?

stable woman

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2013
Posts
3,884
Reaction score
4,479
Habarini??

Nadhani wengi wetu mmekwisha sikia hii habari ya chumaulete hasa kanda hizi za pwani kama tanga na pwani

Hivi majuzi nilikwenda kumtembelea jamaa yangu mmoja anakibanda cha Mpesa, gafla akaja mzee mmoja anataka kuwekewa hela laki tatu kwahiyo akatoa elfu10 thelathini akampa ndugu yangu yule amuwekee hata mimi niliona kuwa zote ni elfu kumikumi akamuingizia laki3

Baada ya hapo sasa ndipo akajakugundua kuwa kaibiwa baada ya kukuta zile hela mahali alipoweka zote ni elfu mojamoja zipo30 kwahiyo jumla yake ni elfu 30.

Ndipo wote tukajiuliza hiki ni kiini macho au ni uchawi?? Hebu tusaidieni wandugu namna ya kujinasua kufanyiwa hivi tena
 
hayo mambo yapo mkuu, huku kusini wanaita chitola au mang'opa. wanadai kama umepokea hela kutoka kwa mtu mwenye tabia hiyo, basi usizichanganye na hela zako nyingine kwa kipindi fulani cha muda, vinginevyo hela zako zote ziatatoweka. hii inawezekana kwa maeneo ya vijijini ambako watu wanafahamiana tabia, kwa mjini ni ngumu kuizuia
 
SAM_0702.JPG
 
Uchawi wa aina hii mbaya sana.Ndo mara ya kwanza nasikia hii .Nashukuru kwa taarifa.
 
hayo mambo yapo mkuu, huku kusini wanaita chitola au mang'opa. wanadai kama umepokea hela kutoka kwa mtu mwenye tabia hiyo, basi usizichanganye na hela zako nyingine kwa kipindi fulani cha muda, vinginevyo hela zako zote ziatatoweka. hii inawezekana kwa maeneo ya vijijini ambako watu wanafahamiana tabia, kwa mjini ni ngumu kuizuia

kwa mjini ni inshu kweli kujua hili
 
Hii inaweza ikawa njia nzuri sana kwa wale wafanyakazi wetu..., wanatuibia kila kukicha wanaleta hesabu ndogo alafu wanasema Chuma Ulete...
 
heee acha bwana hadi kwenye mazao?? Inakuwaje hiyo??
Ni kwamba unaweza kulima sana na mazao yakawa yamekubali (unaweza sifiwa na watu kuwa hautakuwa na tatizo la chakula katika msimu huo!). Tatizo linakuja wakati wa uvunaji. Kiasi utakachopata ni kiduchu sana kwani mazao mengine ni kama unamvunia huyo mwenye dawa! Ni ajabu lakini ni kweli!
 
duh aisee hii nayo kali watu wanapenda kuishi bure kupitia jasho la mwingine
 
Habarini??

Nadhani wengi wetu mmekwisha sikia hii habari ya chumaulete hasa kanda hizi za pwani kama tanga na pwani

Hivi majuzi nilikwenda kumtembelea jamaa yangu mmoja anakibanda cha Mpesa, gafla akaja mzee mmoja anataka kuwekewa hela laki tatu kwahiyo akatoa elfu10 thelathini akampa ndugu yangu yule amuwekee hata mimi niliona kuwa zote ni elfu kumikumi akamuingizia laki3

Baada ya hapo sasa ndipo akajakugundua kuwa kaibiwa baada ya kukuta zile hela mahali alipoweka zote ni elfu mojamoja zipo30 kwahiyo jumla yake ni elfu 30.

Ndipo wote tukajiuliza hiki ni kiini macho au ni uchawi?? Hebu tusaidieni wandugu namna ya kujinasua kufanyiwa hivi tena

Uzi wowote wenye neno " ghafla" kwenye aya ya kwanza huwa ni stori ya kutungwa.
 
hayo mambo yapo mkuu, huku kusini wanaita chitola au mang'opa. wanadai kama umepokea hela kutoka kwa mtu mwenye tabia hiyo, basi usizichanganye na hela zako nyingine kwa kipindi fulani cha muda, vinginevyo hela zako zote ziatatoweka. hii inawezekana kwa maeneo ya vijijini ambako watu wanafahamiana tabia, kwa mjini ni ngumu kuizuia

wewe ni muongo au mbinafsi, kama ulikuwa unajua yote hayo kwanini usinge anzisha uzi? umesubiri mpaka mtu mwingine aanzishe uzi!!! Tabia hii ikomeshwe mara moja, kama unajua kitu, anzisha uzi, sio unasubiri mpaka mtu mwingine aanzishe. Kama stable woman asinge anzisha uzi huu, haya tungeyajuaje?
 
Kwanini hao watu wa chuma ulete wasiende kufanya hayo mambo yao katika mabenki? wangekuwa matajiri sana.
Mi naona ni story tuu kwasababu ukionyeshwa hao wenye tabia hizo mara nyingi huwa ni vibabu ambavyo kiuchumi vina hali mbaya sana pamoja na kuambiwa kuwa hujipatia pesa kwa njia hizo.
 
wewe ni muongo au mbinafsi, kama ulikuwa unajua yote hayo kwanini usinge anzisha uzi? umesubiri mpaka mtu mwingine aanzishe uzi!!! Tabia hii ikomeshwe mara moja, kama unajua kitu, anzisha uzi, sio unasubiri mpaka mtu mwingine aanzishe. Kama stable woman asinge anzisha uzi huu, haya tungeyajuaje?

Kuchangia imekuwa nongwa tena?? Mtu anapoweka wazo lake hapa ni ili anayefahamu alieleze tusiofahamu tupate shule!!

Hiyo ndiyo maana halisi ya kuweka bandiko humu, unaweza ukajua kitu lakini usiwe na wazo la kuanzisha uzi ndugu.
 
Hayo mambo yapo sana na dawa ni moja tu haihitaji uchawi wala kwenda kwa mganga....
Unapoweka pesa zako weka kipisi cha mkaa mweusi tiiii uliotumika kabsa...
Wakifanya hyo michezo tena basi watakua ni zaidi ya noma.....
 
Hee kwahiyo mkaa unasaidia nini??
 
duh aisee hii nayo kali watu wanapenda kuishi bure kupitia jasho la mwingine

Hii ni kweli kabisa tena mchezo huu upo sumbawanga mi kuna ndugu yangu alilima mahindi huko kama heka mbili na yalikubali kweli kasheshe ilikuja kwenye kuvuna hata gunia mbili hakupata!! na mchezo hufanyika pale unapokuwa una vuna ndio nao wanachukua chao,hadi mwaka uliofuta akawaona wazee wa pale wakamwambia dogo ulijifanya mjanja umeona?ndio wakampa dawa kuzungushia shamba lake hadi leo mavuno ni ya kufa mtu!!!!yaani hizi sayansi zingekuwa wazi tungekuwa mbali sana.
 
Back
Top Bottom