Habari wakuu kuna trend ya watu kutishiana vitu mtandaoni bila kujali sheria ya Tanzania inasema vipi.
Unakuta mtu anasema hadharani kamlawiti flani mtandaoni na bado anachekewa kabisa hii haiko sawa kisheria adhabu ya ulawiti ni miaka 30 jela. Miaka 30 sio midogo kwanini upate adhabu ya miaka hiyo??na upoteze maisha na malengo yako kwa kauli za ajabu ajabu??
Mambo ya kulawitiana ndio yamekuwa na nguvu kwenye mtandaoni na wengi wanajipa vichwa hawatajulikana don't fool yourself asee bwana. Mance Mello hawezi kutetea walawiti atatoa info zenu bila wasiwasi.
Na kuna wengine wanatoa kauli za ajabu ajabu na bado namba zao zipo mitandaoni najiuliza ni uelewa mdogo wa sheria ama ni ukubwa wa kichwa kuwa na akili kidogo??
Kwenye miaka hii ambacho technology imepamba moto angalia kauli zako Internet haifuti kitu ukiandika Leo miaka kumi kitakuwepo na kitatumika kukufunga.
Kuweni makini na kauli zenu.
Jioni njema