Mr-Njombe
Member
- Aug 29, 2022
- 64
- 122
Salaamu wanaJF,
Ni matumaini yangu mu wazima, naomba kuainisha mtazamo wangu kuhusu wafuasi na wanachama wa vyama vya upinzani nchini kama ifuatavyo.
TAMU
Asilimia kubwa ya wafuasi wa vyama vya upinzani tanzania wamekua mstari wa mbele kwenye kukemea maovu na kuishinikiza serikali kutengua na kubadili baadhi ya maamuzi ambayo wanadhani kua si sahihi yakitekelezwa kwenye jamii.
Pia kwa wafuasi waliobahatika kua viongozi sehemu tofauti tofauti pia wameleta chachu hasa kwa wale waliokua bungeni kwa kuweza kuhoji bila kupepesa macho baadhi ya miswaada ya sheria, maamuzi ya serikali, utekelezwaji wa sera mbali mbali, ukiukwaji wa katiba n.k
CHUNGU
Hapa ni kwamba wafuasi wengi wamekua wana mwamko sana kwenye mitandao ya kijamii kwa asilimia kubwa kuliko kushiriki moja kwa moja kwenye shughuli za kichama katika ngazi zote . Na hapa inaenda mbali mpaka mikutano ili iweze kua na watu wa kutosha ni lazima iambatishe viongozi waandamizi wa kitaifa, na hivyo ajenda mbali mbali kutegemea mitando ya kijamii kwa sehemu kubwa.
Na kwa kumalizia wengi wamekata tamaa kuanzia kugombea nafasi mbali mbali za uongozi na kususia kujiandikisha katika daftari la kupiga kura ama kwa waliojiandikisha kutojitokeza kuchagua viongozi katika chaguzi za ngazi zote. licha ya uwepo wa malalamiko ya utendaji wa tume laikini ushiriki pia ni duni.
Hitimisho
Uhai na ustawi wa vyama unategemea ushiriki kikamilifu wa wafuasi na wanachama katika nyanja zote ikiwemo katika mikutano, kugombea na kuchagua viongozi ambao wanadhani kwa sera na maono waliyonayo yataleta maendeleo katika jamii.
Naomba kuwasilisha.