Hello! Mambo vipi?
Leo itakuwa siku poa sana kwako kama unasumbuliwa na chunusi au madoadoa usoni yatokanayo na chunusi. Kama husumbuliwi na matatizo hayo sio mbaya pia kwa sababu utajiwekea akiba na kusaidia ndugu, jamaa na marafiki zako.
Unajua kwamba madoadoa ya chunusi kwa kiasi kikubwa yanasabishwa na kupasua chunusi? Pia je, unajua kwamba chunusi huweza kusababishwa na vipodozi vyako mwenyewe ambavyo unatumia hata kama ni salama na vimesajiliwa na mamlaka ya chakula na dawa Tanzania (TFDA)?
Unajua kwamba vipodozi kama Carotone, Caro light, Bronze tone, Extra Clair, Maxi White nk huchangia sana kusababisha chunusi na hatimaye madoadoa?
Kama ulikuwa hujui basi habari ndo hiyo. Kuna mambo mengi zaidi ya hayo na nitaendelea kukuelimisha na kukushauri kadiri muda utakavyoruhusu.
NINI HUSABABISHA CHUNUSI?
Chunusi huweza kusababishwa na kuongezwa na moja kati ya vitu vifuatavyo:
1. Maambukizi ya bakteria wa chunusi
2. Homoni nyingi za uzazi mwilini, ujauzito na dawa za kupanga uzazi
3. Vipodozi vyenye kemikali kali na vile visivyoendana na ngozi yako
4. Vyakula vyenye mafuta mengi na viungo vya kwenye chakula
5. Msongo (Stress)
6. Mafuta mengi usoni
7. Vumbi na uchafu mwingine kuziba matundu ya ngozi (ya kutokea mafuta)
Sawa?
Sasa kama umeelewa hayo basi kwenye kuzuia itakuwa rahisi maana utakuwa unayapunguza au kujiepusha nayo tu (Kwenye ujazuito sijui utafanyeje …… )
JINSI YA KUZUIA CHUNUSI ZISIENEE WALA KUKUACHIA MADOADOA
Zaidi ya miaka mitano sasa tumekuwa tukiwaelimisha na kuwashauri kuhusu ngozi na vipodozi na maendeleo yamekuwa mazuri. Tumekuwa tukikushauri usipasue chunusi, badala yake tumia dawa vizuri na chunusi zitanywea na kukauka zenyewe bila kukuachia vidonda wala madoadoa.
Pia tumekuwa tukikushauri kama unasumbuliwa na chunusi na mafuta mengi basi ni muhimu sana kudhibiti mafuta kwanza kabla ya kuanza kushambulia chunusi kwa nguvu kubwa na kupata matokeo polepole.
Matibabu ya chunusi hutofautiana kati ya mtu na mtu kutegemea na chanzo cha chunusi, aina ya ngozi, umri na mtindo wa maisha hivyo unatakiwa kupata ushauri wewe kama wewe na kutumia matibabu yanayoendana na mazingira yako.
Ukitaka kuzuia chunusi zisienee wala kukuachia madoadoa fanya mambo yafuatayo:
1. Pata ushauri hospitali au kwa mtaalam ili kujua jinsi ya kudhibiti vizuri zaidi chunusi zako na kuanza matibabu haraka. Kama chunusi zako zimesababishwa na bakteria utapewa dawa ya kuua bakteria hao na kukusaidia chunusi zako kuisha haraka badala ya kuenea na kukuachia madoadoa
2. Usipasue chunusi zako, maana kupasua chunusi ni kama kumwagia petrol kwenye moto
3. Tumia face wash/facial cleanser au sabuni za kusaidia kuondoa uchafu na vijidudu kwa ufanisi mkubwa zaidi kuliko sabuni za kawaida. Pia tumia poda kwa ajili ya kukausha mafuta na kukusaidia kuiweka ngozi yako iwe laini.
4. Punguza kiasi cha mafuta na viungo unavyokula – epuka vyakula vyenye mafuta mengi, epuka vyakula vyenye viungo vingi na pikia kwa mafuta na viungo kiasi cha wastani tu
5. Pambana na msongo (Stress). Hii haitakusaidia katika kudhibiti chunusi tu bali hata kwenye magonjwa ya moyo, presha, sukari, akili, vidonda vya tumbo, nguvu za kiume na kadhalika.
6. Acha kutumia vipodozi vyenye sumu na pia usitumie vipodozi visivyoendana na ngozi yako. Hii watu wengi wenye ngozi ya mafuta wamekuwa wakikosea sana kwa kutumia losheni au mafuta kwa ajili ya ngozi kavu na hatimaye kutokwa na vipele na chunusi kuongezeka.
Unaona? Mambo ni rahisi tu kama hivyo na ndani ya wiki moja tayari unaanza kufanikiwa kudhibiti chunusi zako.
Sasa kazi ni kwako kuchagua – kuendelea na mazoea au kufuata ushauri wa kitaalam.
AFYA ZAIDI (AZ) CONSULTANTS tunakushauri uachane na stori za kitaa na ufuate ushauri wa kitaalam. Pia usile kila kitu unachokutana nacho mtandaoni, vingine sio kwa ajili yako.
Uwe na siku njema!
Kama unatumia whatsapp na ungependa kupata madarasa ya afya, urembo na vipodozi; orodha ya vipodozi visivyo salama; matatizo ya ngozi nk basi tucheki tu kwa namba 0719326693 na tutakutumia. Free for you!
Pia kama unahitaji kujifunza zaidi kuhusu afya, urembo na vipodozi kila siku hadi mwisho wa mwezi basi tutumie meseji whatsapp kwa namba hiyo hiyo na kisha tutakutumia link ya kujiunga na group letu la whatsapp na utapata elimu na ushauri zaidi. Free for you!
Kama unasumbuliwa na tatizo (afya, urembo au vipodozi) na unahitaji kuondokana nalo sasa tupigie simu au tutumie meseji au whatsapp na tutakushauri pia. Mawasiliano ya haraka ni 0743422883 na 0719326693; email ni
afyazaidi@gmail.com
See you next time!