Chunusi: Chanzo, tiba na jinsi ya kuepukana nazo

Chunusi: Chanzo, tiba na jinsi ya kuepukana nazo

Jinsi ya kuondoa chunusi usoni kwa njia ya asili fuata hatua hizi.

1. Mdalasi na asali ndio mahitaji yetu
Tumia mchanganyiko wa asali na mdalasini wa unga kwa kupaka angalau mara moja kwa siku. Asali na mdalasini zinasaidia katika uponyaji kwa sababu zina ‘anti-bacteria’ (zinaua na kuzuia bacteria)

Jinsi ya kufanya:

• Chukua asali kwenye kipimo cha vijiko vitatu vya chai

• Chukua mdalasini wa unga kwa kipimo nusu kijiko cha chai

• Changanya pamoja

• Paka sehemu yenye chunusi na kisha kaa na mchanganyiko huo kwa angalau dakika 10-30 kisha osha kwa maji ya uvuguvugu, mdalasini unaweza kuwasha kwenye ngozi hivyo unashauriwa ujaribu kupaka kidogo kwenye kiganja cha mkono kwanza ili kupata uhakika kua haitakusumbua.
 
Wengine tuna chunusi kama maganda ya fenesi.

..............Acha tujaribu hii huenda ikatusaidia.
 
JINSI YA KUONDOA CHUNUSI USONI KWA KWA HARAKA ZAIDI.

Na:Mr tibalishe

Chunusi ni vipele vinavyojitokeza katika ngozi hususan sehemu za usoni, kifuani na mgongoni kutokana na mafuta kushindwa kutoka kwenda nje ya mwili (juu ya ngozi ya nje). Huweza kutokea kwa mtu yeyote aliyepevuka kimwili, japokuwa wanawake hutokewa zaidi na vipele hivi.

SABABU ZA CHUNUSI
Sababu kubwa ya chunusi ni kukaa kwa mafuta chini ya ngozi ya nje na kusababisha uvimbe. Hii inatokana na mafuta hayo kuzalishwa kwa wingi zaidi au kushindwa kupita kwenye matundu ya kutolea mafuta kwa sababu matundu hayo yameziba.
Pia bakteria wa chunusi huweza kushambulia ngozi na kusababisha chunusi au kuzifanya chunusi kuwa nyingi zaidi na kubwa kubwa
Vitu vinavyosababisha au kuongeza ukubwa wa chunusi ni pamoja na
1. Kiasi kikubwa cha mafuta kwenye ngozi
2. Kuziba kwa matundu ya kutolea mafuta kwenye ngozi
3. Homoni za uzazi mwilini (Androgens)
4. Msongo (Stress)
5. Maambukizi ya bakteria wanaosababisha chunusi
6. Kemikali (vipodozi) kali au zisizoendana na ngozi ya mtu
7. Aleji (Mzio) kwa baadhi ya vipodozi na kemikali zingine
8. Baadhi ya vyakula (vinavyotokana na maziwa, chipsi na chokoleti)

NINI CHA KUFANYA?
Ukitokwa na chunusi cha kwanza hakikisha unakuwa mwangalifu ili usiziongeze zaidi. Tafuta sababu insayozisababisha na kisha iepuke au iondoe hiyo kwanza
Cha pili epuka kupasua chunusi. Kupasua chunusi husababisha makovu chunusi zitakapopona
Tatu tafuta matibabu na uanze matibabu mapema. Ni rahisi zaidi kutibu chunusi ukiziwahi kuliko ukiwa umechelewa

MATIBABU YA CHUNUSI
Matibabu ya chunusi hutegemea na ngozi ya mtu na chanzo kinachosababisha hizo chunusi. Matibabu hayo mara nyingi hulenga kuua bakteria wanaosababisha chunusi hizo, kupunguza mafuta na kuzibua matundu ya kutolea mafuta ili mafuta yaweze kupita na kwenda nje ya ngozi.

1. Kuua Bakteria wanaosababisha Chunusi
Bakteria hawa huuliwa kwa kutumia dawa za kuua bakteria zijulikanazo kama Antibiotics. Utaalam na umakini unahitajika katika matumizi ya dawa hizi Pia ni lazima zitumike kwa maelekezo ya daktari

2. Kupunguza mafuta juu ya ngozi na kuondoa mafuta yaliyoziba matundu ya mafuta
Hii ni njia kubwa sana na rahisi ya kukabiliana na chunusi. Kwa kuwa mafuta ni sababu kuu kwa watu wengi basi njia hii husaidia watu wengi sana.
Hili huweza kufanywa kwa kutumia
- Sabuni za PROTEX (Iliyoandikwa DEEP CLEAN) na PEARS (Iliyoandikwa OIL CLEAR)
- Poda ya POND’S (Iliyoandikwa OIL CONTROL)
- Sabuni za maji za kusafishia uso na kuondoa uchafu na mafuta ya ziada (Face Wash au Facial Cleansers)

3. Kuondoa uchafu wote na seli zilizokufa na kuziba matundu ya kutokea mafuta kwenye ngozi
Njia hii hufanya kazi vizuri sana pia. Uchafu huo na seli zilizokufa zikiondolewa mafuta hupita vizuri na kwenda nje ya ngozi bila kusababisha chunusi. Matokeo yake mtu hupona chunusi na pia kuzizuia zisijitokeze.
Hili hufanywa kwa kutumia dawa zinazoondoa utando wa uchafu na seli zilizokufa zilizopo juu kabisa ya ngozi.
Mifano yah ii ni Persol Gel

MUHIMU:
- Ili kudhibiti vizuri chunusi na kuziondoa kabisa unahitajika kujua kwa usahihi kabisa chanzo cha chunusi hizo na vinavyoziongeza
- Mara nyingi chunusi hutibiwa kwa kutumia zaidi ya dawa moja au kipodozi kimoja. Jua vizuri mchanganyiko wa dawa na vipodozi vya kutumia
- Tumia dawa na vipodozi vinavyoendana na ngozi yako. Tofauti na hapo chunusi zitaongezeka zaidi
- Kutibu chunusi vizuri na kwa usalama kunahitaji muda. Kuwa mvumilivu na tumia vitu vyote kama ulivyoelekezwa
- Usipasue chunusi. Utabaki na makovu ambayo nayo pia yatakusumbua

Kwa maelezo zaidi, ushauri na matibabu ya Chunusi, Makovu, Madoa, Mafuta mengi usoni.
SHARE MARA NYINGI UWEZAVYO MUNGU ATAKUBARIKI
 
Mi nadhan hizo ni umri mm enzi za utoto zilikuwa hazinikauki na Kila mafuta nilipaka.. lkn Sasa Wala nipo fine tu
 
tumia dodoki uwe unajisugua usoni kila ukioga, utakua soft tu, mm ndio nafanya hvyo chunus zote zimeisha
 
Chunusi husababishwa na mafuta yaliyo kwenye ngozi, kikubwa cha kufanya usiangaike na dawa za kuondoa chunusi za aina yoyote ile make unaweza jikuta unaongeza tatizo zaidi. Solution ni kwamba unapoenda kuoga paka sabuni usoni ambayo sio medicated kisha subiri mpaka ikauke baada ya hapo osha kwa maji safi kisha usipake mafuta aina yoyote ile baada ya wiki moja utaanza kuona matokeo mazuri.
 
Mimi ni muhanga wa chunusi. Zilinitesa sana hamna dawa ambayo sijatumia. Ingekua sehemu ambayo hatufichi identity zenu ningekutumia picha za before and after ili u prove. Kuna dawa nilitumia ukienda duka la dawa utapata. Chunusi zako ni white heads au black heads? What is the extent of the problem. Tuma picha hata la shavu tu nione.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1. Kunywa maji mengi ya kutosha kila siku , atleast 1.5 lt and above.
2. Fanya mazoezi ya mwili kila siku.
3. Kula mbogamboga na matunda kwa wingi.
 
Back
Top Bottom