Chunusi yaua kijana Tanga

Chunusi alikua ananichanganya nilipokuwa mdogo maana naambiwa anaua Sasa nikawa nashangaa mbona dada yangu anachunusi na hafi
 
Huyo mvuta bangi tu,usichanganye bangi na maji.
Alishaanza kuvua nguo hata baharini hajafika
 
 
Chunusi anatisha lakini sitoacha kamwe kuogelea lake Tanganyika bangwe beach,Mto Mbulumi Moro,bahari ya hindi coco na mto karanga..
 
kwa waliokaa moshi kuna msitu ukielekea langoni kuna sehemu mto rau unapotea machoni sasa pale unapopotea mbuzi wengi walikwenda pale akianza kuzama ukijaribu kumuokoa wote mnakwenda kusalimia kusikojulikana na tutakufuata baada ya siku tatu au mbili samaki wakiwa wamejiburudisha macho na viganja vyako.na nimeshuhudia tukiwapoteza ndugu zetu waili pale lake duluti baada ya msichana rafiki yetu aliitwa hadija kuanguka kwenye kiboti sasa mshikaji akiitwa Azza akajaribu kumuokoa mpaka leo imebaki stori tuliipata miili yao asubuhi yake.
 
Hizi habari nakumbuka kambi ya Mgambo JKT ya Kabuku, Tanga. Kuna bwawa kubwa hilo kipindi tupo mafunzoni tuliwahi kusimuliwa lina chunusi, ambapo wanajeshi wenyewe njia ya kwenda bwawani wameweka bango kutoa onyo mtu asiogelee ni hatari.

Ruksa kuchota maji ya kumwagilia tena mwanzoni tu sehemu yenye maji ya ugoko. Unaambiwa ukitaka kuoga chota kaogee mbali, aliyejaribu kuingia ni mwanajeshi mmoja wa kipindi cha nyuma. Ulikuja kuonekana mwili wake unaelea baada siku tatu.

Haya mambo yanatatanisha sana, sijawahi kuyaona kwa macho ila kwa yanatokea lazima niwe na shaka aisee. Wanajeshi wenyewe wakwambie, ukiogelea hurudi
 
mambo kama haya yapo sana maeneo ya pwani; nimekutana nayo mtwara na lindi pia
 
Huyu jamaa alikuwa anaoneshwa kitu gani kitatokea ila sasa hakuwa na namna ya kukataa kwenda mana kifo kikipangwa lazima uende tu ila siamini sana kuhusu chunusi
 
Mvuvi maarufu na mtaalamu wa mambo ya bahari na mito, bwana Hmood Nassor Hamdoun anaeleza dhana moja ndegefu inaoaminika na wengi hasa wa mwambao mwa pwani kwamba baharini kuna jini liitwalo Chunusi.

Akitumia picha tanzu bwana Hmood anasema, katika picha anaitwa chunusi ila kwa jina lingine anaitwa "electric eel". Anafanana na kambale. Anatoa umeme wa aina ya tuli (static electricity) hadi vilt 850v.

Kiwango hicho cha umeme kinatosha vizuri kuua binaadamu na damu kuganda ndio maana utasikia wanasema jini chunusi ananyonya damu.

Ni vigumu kumvua kutokana na maumbile yake na umeme autoao. Wengi hawajawahi kumuona ndiyo maana inabaki kuwa tu ni jini wa kwenye maji.

La Voice ni muafrica wa kwanza kugundua kuwa chunusi sio jini bali ni electric eel.

___________________
Kupanua ufahamu wako zaidi, endelea kufunua kurasa za kitabu pendwa cha Taifa cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi.

Nunua kitabu cha Ujasusi kwa @ 80,000/= popote ulipo.

Lipia 80,000 kwa 0715865544 au 0755865544 (Yericko Nyerere) kisha tuma majina yako na mahali ulipo. Nje ya Dar utachangia nauli
Cc @yericko nyerere

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Daah hiii story inanikumbush kifo cha ndugu yang paskal aisee kama ningekuwepo hy siku tungekufa wot nisingekubal kuacha kamand wang apotee.. inasemekan alikuw ni chunus , waokoaj walimtafut bila mafanikio akakutw asubuh ngozi ya paja imechunwa damu zimetoka mpk zimgandian kiukwl it was very bad day for me lile bwawa had Leo nalichukia
 
Kwaio mkuu umeme tuli ndo unasifa ya kufany mtu asionekan siku tatu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…