Chunya, Mbeya: Mtendaji wa kijiji adakwa kwa tuhuma za mauaji

Chunya, Mbeya: Mtendaji wa kijiji adakwa kwa tuhuma za mauaji

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2021
Posts
577
Reaction score
2,595
Mbeya. Jeshi la Polisi mkoani hapa linamshikilia Mtendaji wa Kijiji cha Sangambi Wilaya ya Chunya Joseph Nangale (45) kwa tuhuma za mauaji ya Aron Mbuba (18).

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga amesema tukio hilo lilitokea Septemba 17 mwaka huu baada ya marehemu kupigwa na kitu butu kichwani.

"Siku hiyo Nangale akiwa ameongozana na askari mgambo wawili wa kijiji walimkamata Mbuba wakati wakiwa kwenye msako wa wauza mkaa bila kulipa ushuru wa kijiji.

"Wakati wanamkamata aliwajibu “hana hela” ndipo mtendaji wa kijiji na Askari Mgambo walimpiga sehemu mbalimbali za mwili na baadae kumuweka mahabusu ya kijiji hadi Septemba 19 baada ya kudhaminiwa."

Hata hivyo kutokana na kuwa na maumivu makali, Mbuba alienda kupatiwa matibabu katika Zahanati ya kijiji hicho lakini siku iliyofuata (Septemba 20) alifariki dunia kutokana na majeraha aliyoyapata kwa kupigwa.

Jeshi la Polisi linaendelea kuwasaka watuhumiwa wengine (Mgambo) ambao walikimbia mara baada ya tukio hilo.

"Nitumie nafasi hii kutoa rai kwa wananchi na viongozi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi pindi wanapowakamata watuhumiwa kwa tuhuma mbalimbali na badala yake wajenge tabia ya kuwafikisha kwenye mamlaka husika ikiwa ni pamoja na vituo vya Polisi kwa hatua zaidi za kisheria."

Chanzo: Mwananchi
 
Kibao kimegeuka, watanyea debe hadi 2050

Cheo ni dhamana!
 
Chunya mauaji mengi juz kati kuna mfanyabiashara wa alizeti walimuua wale jamaa kukamatwa wameonyesha walipomuulia na mabaki ya watu wengine waliowaua.
 
Nchi hii imekuwaje tena,kila mwenye mamlaka basi anayatumia awezavyo.Ni mauaji tu kila kona ya nchi.
 
Nazani Kuna shida ya uandishi apo kwenye taarifa. Tukio lilitokea September 17, akawekwa mahabusu Sept 19, akafariki Sept 20. Au me ndo sijaelewa ndugu.
 
Back
Top Bottom