Chuo cha Afya Mac Wish kinakwama kwenye Marekting bila kufahamu

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,236
Reaction score
10,774
Ni jambo la kushangaza kuona taasisi ya elimu kama Chuo cha Afya Mac Wish ikishindwa kunufaika na fursa ya kujitangaza ipasavyo. Badala ya kuwa na kitengo cha masoko chenye ubunifu na mvuto, kimeonekana kutochukua hatua madhubuti – na matokeo yake, majukumu nyeti ya marketing yameachwa mikononi mwa watu wasiokuwa na taaluma ya kazi hiyo.

Mfano wa hivi karibuni ni “homeboy” kutoka Rukwa, ambaye badala ya kueleza ubora wa chuo, kozi zinazotolewa, uhusiano wake na soko la ajira, au mafanikio ya wahitimu wake, amejikuta akisimulia hadithi za kufika chuoni mapema na “kuweka rekodi.” Ni dhahiri kuwa simulizi za namna hii haziwezi kumshawishi mzazi au kijana kuchagua chuo fulani, hususani katika zama ambazo ushindani wa vyuo vya afya nchini ni mkali.
Your browser is not able to display this video.

Maswali muhimu yanabaki: je, uongozi wa Mac Wish unaona haja ya kuwekeza kwenye timu ya marketing yenye weledi, au wataendelea kukabidhi hadhi ya chuo kwa simulizi zisizo na tija? Wataalamu wa masoko wanashauri kuwa kitengo cha marketing si hiari tena bali ni uti wa mgongo wa taasisi yoyote inayotaka kushindana na kuishi.

Mac Wish ikichelewa kuamka, vyuo pinzani vitashinda mbio za kuwavuta wanafunzi bora. Ila hongera sana homeboy kwa kuweka rekodi.
 
Mkuu umefukuzwa hapo au ? Support hustle za vijana wakiTanzania.
 
Chuo kinamilikiwa na vijana wadogo wanaopambana. Ni wasikuvu na watu wema tu. Ungeenda kuwaona na kuwapa maono yako na kuwasaidia kutengeneza marketing strategy nzuri lingekuwa jambo jema sana.
 
Kiswahili hajui
Kiingereza hajui pia

Macwish college of es ende alaidi sayansi (badala ya health anasema es)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…