robbyr
Senior Member
- Apr 8, 2017
- 129
- 221
Picha: Mtandaoni
Kwa heshima kubwa nampongeza rais na baraza la sanaa kwa kuona kuna kitu tunaweza kujifunza kutoka kwa jamii ya watu wa Korea Kusini
Ila niseme kuwa wizara ya sanaa imeshindwa kutafsiri maono ya rais juu ya sanaa yetu.
Ila wasani hawaendi kujifunza utamaduni wa Korea ili waje kuigiza hapa Bongo. Nahisi wengi watatumia kama sehemu ya kutalii
Limefanyika kosa kupeleka wasani korea bali Serikali ilipaswa kuwekeza kwenye chuo cha sanaa kwa kuajiri wataalamu wa sanaa kutoka korea ambao watafundisha uandishi bora wa stori na kuchukua muvi.
Kazi iwe kwetu kutumia taaluma hiyo kuandika stori zenye ubunifu wa mafunzo kutoka Korea unao akisi utamaduni wetu.
Pia, kuna naona walioenda Korea wengi ni wazee ingali kuna vijana walistahili maarifa hayo ili wawe chachu ya mabadiliko ya sanaa hapa nchini hapakuwa na malengo ya muda mrefu ya baraza la sana au wanataka kumfurahisha rais.
Hivyo, Hakuna haja ya baraza kupeleka wasani Korea bali kuwe na Darasa bora kwenye chuo cha Sanaa Bagamoyo na kuajiri wataalamu toka nchi mbalimbali kama tuna malengo ya muda mrefu wa kukuza sanaa yetu. Na pia watu wasome kwa vitendo na wahitimu
PIA SOMA
- Rais Samia Suluhu awasili nchini Korea Kusini kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Korea, Yoon Suk Yeol