KERO Chuo cha City College (Kigamboni) kinatuzungusha tuliosahihisha mitihani yao

KERO Chuo cha City College (Kigamboni) kinatuzungusha tuliosahihisha mitihani yao

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Taasisi ya Chuo cha City College Mikwambe kipo Kigamboni, Mikwambe, Dar es Salaam., walituita kufanya kazi ya kusahihisha mitihani na walisema wangetulipa baada ya kazi kuisha, lakini tangu mwezi wa saba 2025 leo Machi 2025 hatujalipwa malipo yetu.

Tukiwatafuta hawana majibu ya kueleweka, mbaya zaidi wameamua kulipa baadhi ya watu ambao wameitwa tena kusahihisha mitihani ya term hii.

Sisi Mithihani tuliyosahihisha ni joint examinations kutoka campus zao zote za Dar, Dodoma, Arusha na Mwanza.

Walimu wapo chuoni kwao lakini mithihani ikiwa mingi especially kwa joints exams inawalazimu kuomba watu waende kusahihisha kwa makubaliano ya kulipana baada ya kazi kuisha kwa sababu mithihani inakuwa mingi na hao hao walimu inabidi wafundishe na at the same time wasahihishe so wanazidiwa ndio mana tuliitwa.

Mkuu wa chuo anaitwa Boaz, ameamua kutu-block na simu zetu hawapokei, meseji ndio kama hivyo wanajibu wanavoona wao na chuo tulishaenda hakuna lolote.

Ahadi zao ndio zilezile wanafatilia, kumbe wametuweka pending na kazi zao zinaendelea. Sisi tunataka watulipe tu pesa zetu.

Sisi hatuna kituo, ila inapotokea kazi wanapigia watu simu tunaenda.

Sisi ni wafamasia. Na ndio mana tunasahihisha mithihani ya PST tu ambayo ni ya wanafunzi wa famasi.
 
Sio kuwa fedha hizo huwa zinalipwa na Baraza la wafamasia?!!
 
Hivi inakuwaje unaelewana na watu vizur tu hlf unakuja kuwageuka baadae?
 
wangetulipa baada ya kazi kuisha, lakini tangu mwezi wa saba 2025 leo Machi 2025 hatujalipwa malipo yetu.
tangu mwezi wa saba 2025 leo Machi 2025 hatujalipwa malipo yetu. 🤔🤔
 
Back
Top Bottom