DOKEZO Chuo cha City College kimeahirisha mahafali ghafla baada ya wanafunzi kulipia majoho

DOKEZO Chuo cha City College kimeahirisha mahafali ghafla baada ya wanafunzi kulipia majoho

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Chuo cha City College kimewaaacha njia panda wanafunzi waliohitimu masomo yao Mwaka huu 2024 baada ya kutangaza kuwa mahafali( graduation) yatafanyika tarehe 22/11/2024 na kuwahimiza wanafunzi kulipia majoho kiasi cha shilingi 50000/= kwa dead line ya tarehe 12/10 baada ya wanafunzi kufanya malipo hayo kwa haraka ghafla wametangaza kuahirisha mahafali bila kutoa tarehe ya mahafali hayo yatakuwa lini.

Tabia ya ubabaishaji kwa chuo hiki haijaanza leo hasa kwa campus za Dodoma na Mwanza. Tunaomba serikali iingilie kati maana tunafahamu tabia yao wakianza ubabaishaji huu mwisho wa siku tutasubiri sana.

Pia baadhi ya wahitimu wanalalamika tayari wameshafanya booking za usafiri. Mahafali hayo yalitakiwa kufanyika Mwanza huku kampasi zote zikiwa zinatarajia kukutana huko Mwanza.

c1.jpg
c2.jpg
 
Wanafunzi waliohitimu mafunzo ya utabibu katika chuo cha City College bado wanalalamika kwa huzuni baada ya chuo hiko kukusanya pesa za majoho na kutokomea nazo kwa kukaa kimya na kufunga group la whatsApp lililokuwa linatumika mwanzo kwaajili ya mawasiliano kati ya wahitimu hao na waratibu wa hayo mahafali.

Chuo hiki kilifanya ujanja unaofanana na wizi wa mtandaoni wa kutoa taarifa rasmi ya mahafali kuwa ni tarehe 22/11/2024 na dead line ya kulipia majoho ilikuwa tarehe 12/11/2024( narekebisha taarifa iliyopita nliandika tarehe 12/10/2024) na baada ya wahitimu kulipa ghafla wakabadilisha na kutoa sababu nyingi kuwa mahafali yamehairishwa?

Kwanini huu ni utapeli?
1: Mpaka walipotangaza tarehe ya mahafali maana yake walikuwa wameshakaa chini nakuona kuwa hiyo tarehe haitoingiliana na ratiba nyingine

2: Walikuwa wanahimiza sana kulipa kwa haraka
3: Mpaka sasa waliokuwa wanahimiza kuhusu kulipia wamekaa kimya na hakuna taarifa yoyote
4: Njia ya mawasiliano kati ya wahitimu na waratibu wa graduation (WHATSAPP group ) wamefunga ili kukwepa maswali.

Mamlaka husika tunaona muongee na hiki chuo ili wahitimu wapate angalau taarifa nini kinaendelea ikiwezekana pesa zirudishwe wahitimu watachangia muda ambao chuo kitakuwa kimejipanga.
 

Attachments

  • Screenshot_20241116_150330_WhatsApp.jpg
    Screenshot_20241116_150330_WhatsApp.jpg
    483.4 KB · Views: 5
Back
Top Bottom