DOKEZO Chuo cha Kampala tawi la Dar Es Salaam kinafanya ’janja-janja’ katika kozi za Udaktari. Mamlaka na TCU njooni mfanye Uchunguzi

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Tumeishaaa. Sasa hawa ndio baadae waje kututibu nashauri hivi vyuo uchwara vya udaktari vyote vifungiwe maana wengi wanaoenda hapo ni mafailure udaktari si lelemama...vibaki Muhimbili,cuhas na kcmc.
 
Dkt. Gwajima D
 
Ufaulu wa wanafunzi unazidi kuongezeka tena wa masomo ya science ila vyuo vyote vikongwe miundombinu yake na uwezo wa kuchukua wanafunzi hususani kozi za Afya ni Ile Ile miaka yote,Chuo cha kimataifa cha kampala Tanzania kina mapungufu mengi kama yalivyoainishwa ila ndio chuo kilichothubutu kwenda na kasi huu ufaulu mkubwa wa sasa nchini pia kimekua kimbilio kwa wanafunzi wengi ambao wana ufaulu mkubwa lakini wamekosa nafasi kwa vyuo ambavyo haviendani na kasi wa huu ufaulu wa sasa.yote kwa yote changamoto zilizoelezwa Zina mashiko hivyo chuo kinapaswa kiajiri wataalam wakutosha ili waendane na namba ya wanafunzi wanaodahiri.
 
Huo ni uhuni, waliofeli wafanya sup wao.
 
Sasa kinathubutu kwenda na kasi ya udahili wakati kina miundombinu hafifu?

Furaha yako ni kuona wanadahili sana lakini hakuna kitu vijana wetu wanapata sio?!

Grow Up, tuachanane na mambo ya kufurahisha mamlaka, eti kinadahili sana.

Tukiwa Watanzania, kwa umoja wetu, vyuo vya namna hii tunatakiwa kuvipinga bila kujali itikadi zetu.

Ndio maana tunaona vijana wetu hawana uwezo wa kujisemea na kujisimamia katika kila nyanja.

Ukiua elimu, umeua msingi wa Taifa.
 
Soma kijana awamu hii amna mtu atae wasaidia kwenye matatizo kama haya ili hali wanao takiwa kuwasaidia wana mengi yame washinda labda ingekua ile awamu .

Especially icho chuo kina mikono ya watu wazito nisiongee sana ...
 
Kama mmefeli ni halali tu kurudia mtihani usitake public sympathy na wakati umefeli mtihani. Hatuwezi kuwa na Taifa la mambumbumbu..

Kampala kwa MD mimi binafsi naona bado. Nguvu kubwa inahitajika pale kuna shida kubwa.
 
Ndio maana watu wanakipingaga sana hiki chuo!
 
Finally naona uzi kukihusu hiko chuo,
Hopefully watajitokeza wengi kukiongelea 🙌
 
Dr andika barua wapelekeeni TCU kwa ushahidi wako huo itakua nzuri zaidi au unaogopa watakula kichwa ?
Hiyo ni ngumu kufanya.
Alivyofanya ni sawa kabisa...mpiga filimbi!

Madhara ya wahudumu wa afya wenye kiwango duni cha elimu tutayapata sisi wagonjwa.
Serikali ichukue hatua za haraka.
 
Future Dr. pole sana kwa usumbufu uliojitokeza naamini TCU wataliona na kulifanyia kazi.
 
Pole Sana , ngoja tusubiri upande wa chuo watie neno ili tuangalie tunakusaidiaje kijana wetu wa Kampala✊🏿
 
Mkuu mbona unapotosha Umma!! Kuhusiana na kuchukua wanafunzi wengi hilo inaruhusiwa kama una facilities zaidi ndio maana wanao comfirm idadi ya wanafunzi waliodahiliwa ni TCU wenyewe, ukiona wamechukua mwanafunzi 300 ujue TCU ndo wameruhusu kulingana na uwezo wa chuo.

Idadi ya walimu hii sio kweli, Kampala tunafundishwa sana mpaka tunaomba vipindi vingine tuachiwe free!! Wewe unasoma Kampala ipi?

Kuhusiana na matokeo hiyo ni issue personal kati ya mwanafunzi na Department husika. Wewe wakati unalalamika hivyo kuna mwenzio anafurahia matokeo aliyoyapata. Hii sio Kampala tu vyuo vyote. Huwezi kufutiwa matokeo bila sababu.

Wewe una issue zako binafsi ndo zimefanya matokeo yako kufutwa. Sio kitu cha ajabu kufanyika kwenye chuo chochote kinachozingatia sheria za chuo
 
Sasa unaposhauri watu wengine wasisome Kampala mbona wewe uko Kampala?
Ningekuona mtu wa maana Kama ungejikita kushauri paboreshwe ili watanzania wengi zaidi wapate nafasi ya kuelimika katika kada hiyo nyeti ya afya, bandiko lako limejaa fitna na majungu na by principle ukianzisha fitna Ni lazima ikurudie na kukubomoa hata wewe uliyeanzisha...,serikali inaweza kuipiga chini Kampala halafu mtaenda wapi wakati hutaki kusoma darasa la watu 300?
 
UONGO UONGO
 
Kwa kulalamika huko nyie ndio mnaingia vyuon na mentality ya chuo Bata, mwisho ukishikwa pabaya unaaza kulialia
 
Huu ni Upotoshaji na uongo ulijaza fitina za waziwazi Wanafunzi tunafundishwa hadi tunaomba VIPINDI vipunguzwe..

Inawezekana wewe umedisco au umeshindwa Kusoma unapotosha Umma..
Kama una Changamoto ya Kimatokeo Kuna taratibu zimewekwa zifuatilie kuliko kupotosha Umma wa watanzania.
Sisi tuko KIUT, Chuo hakijawahi kufanya maamuzi bila kufuata kanuni na Taratibu zilizopo.
Kama umefeli usitake kuchafua Wenzako

Walimu wapo wa kutosha na uzoefu wa Mda mrefu. Professors na Dkt wa kutosha..!

Ninapingana na wewe una Nia Ovu, unachosema ni Uongo.

Kampala International university in Tanzania. Ni chuo Bora..!
Njoo tusome acha kutafuta huruma.
 
Hapa nakupa mkono mm niliwah kua mwanafunzi wa chuo cha kampala na nimehitumu mwaka jana clinical medicine, kusemq ukweli hakuna chuo kinachokosa changamoto hata mwaka jana zilikuwpo lkn naskuru chuo kilitusaidiq kuzitatua na zikatatulika tulipambana na tukahitaj haki yetu na tumemaliza na kufaulu sasa huyu alooqndika huu ujumbe anakichafua chuo ...wanafunzi wengi hatupendi kusoma na tunaishia kusema tumezulumiwa....kama kweli amezulumiwq mtafteni mumuhoji huyu alooandika atawaambia na mtaona eye ndio mungo.. kampala ndio kuna change changamoto ila wanajitahidi kuzitatua, but kuna changamoto pia.

So mm sipo kwa mwanafunzi wala kwa chuo cha kukushauri kama umezulumiwa haki zenu pambaneni mpat3 haki mtamaliza kama hamjazulumiwa imeenda iyo
 
Hapa nakupa mkono mm niliwah kua mwanafunzi wa chuo cha kampala na nimehitumu mwaka jana clinical medicine ...kusemq ukweli hakuna chuo kinachokosa changamoto hata mwaka jana zilikuwpo lkn naskuru chuo kilitusaidiq kuzitatua na zikatatulika tulipambana na tukahitaj haki yetu na tumemaliza na kufaulu sasa huyu alooqndika huu ujumbe anakichafua chuo ...wanafunzi wengi hatupendi kusoma na tunaishia kusema tumezulumiwa....kama kweli amezulumiwq mtafteni mumuhoji huyu alooandika atawaambia na mtaona eye ndio mungo.. kampala ndio kuna change changamoto ila wanajitahidi kuzitatua ...but kuna changamoto pia ...so mm sipo kwa mwanafunzi wala kwa chuo cha kukushauri kama umezulumiwa haki zenu pambaneni mpat3 haki mtamaliza kama hamjazulumiwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…