DOKEZO Chuo cha Kampala tawi la Dar Es Salaam kinafanya ’janja-janja’ katika kozi za Udaktari. Mamlaka na TCU njooni mfanye Uchunguzi

DOKEZO Chuo cha Kampala tawi la Dar Es Salaam kinafanya ’janja-janja’ katika kozi za Udaktari. Mamlaka na TCU njooni mfanye Uchunguzi

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Chuo cha kampala kinadahili wanafunzi wengi kuliko capacity yake. Kwa mfano sisi mwaka wa kwanza ilitakiwa wachukue wanafunzi 150 tu lakini walichukua watu Mia tatu na kitu

Pili hakina walimu wa kutosha kwa kozi ya shahada ya udaktari wa binadamu, paediatrics kuna mwalimu mmoja tu, gynecology kuna mwalimu mmoja tu, hivyo inapelekea kutahiniwa na mwalimu mmoja hata clinical exam kitu ambacho si sawa.

Tatu na ambayo ndo shida haswa ni kuhusu matokeo ya mitihani ambapo wamefuta matokeo ya semester 1 ya mwaka wa 3 bila sababu za msingi eti turudie mtihani wakati tulishafanya na matokeo yakatoka yakiwa na massive failure kwa sababu hatukufundishwa. Sasa tupo semester ya pili na tuna week 6 tu kumaliza hii semester lakini wanataka tuanze kusoma masomo ya semester waliofuta matokeo alaf tuje kufanya oral viva ili watupe marks hii sio sawa hata kidogo.

Muda ni mchache huwezi kusoma masomo yote manne ndani ya week 6 na ukafaulu mtihani yaani usome pediatrics, internal medicine, surgery na obs and gyn, hii ni unfair na sio utaratibu kwa maana waliofeli wafanye sup zao na waliofaulu waendelee mbele.

Sasa kama mtu alifaulu na sasa akafeli watarudia tena kufuta matokeo?

Hii sio sawa na Kampala imekuwa na tabia za kujiamulia kufanya wanavyotaka wao. Maana nasomaje semester ya pili wakati sija qualify semester 1.

TCU na Wizara ya Elimu njooni KIU kuna madudu mengi sana.

Mwisho siwashauri watu kusoma chuo cha Kampala
Hilo suala la kusema kindahili wanafunzi wengi hio ni uwongo ......hakuna chuo kinachodahili wanafunzi wengi maanq mwanachuo hawez kua mwanachuo bila kupitishwa na bodi za afya na confirmation kule nacte au tcu ...watu wakiwa wengi nacte au tcu wanareject ....lkn pia kuhusu waalimu wa obgy ..paedi ..surgery..Rch anatomy..gyna wapo wengi sana naweza ata kuwataja hapa ....usichafue chuo broooo na usipotoshe watu ....
 
Mkuu inaonekana umedisco bila hata ya kwenda club, Sasa Mkuu tumia muda huu kurekebisha ulipojikwaa, Acha kuchafua Taasisi za watu, unalalamika chuo hakifai lakini hapo hapo na wewe umeenda hapo hapo, Hii ni ishara kubwa kuwa vyuo vingine vikubwq kama Muhimbili, KCMC uli disquality kipindi cha ku apply
 
Back
Top Bottom