christophermmassi
New Member
- Jul 8, 2024
- 3
- 3
Mwaka 2019 chuo chetu kilipata janga la kuungua moto na Vyeti vyetu wanafunzi wahitimu 43 vikaungua, Tangu wakati huo tumepata usumbufu wa kutopata vyeti vyetu kutoka Chuo na NACTVET huku wote wakirushiana mpira kwa kusema ni uzumbe wa mwingine mpaka sasa sisi kutokupata vyeti vyetu.
Tunaomba JamiiForums kusaidia wadau mbalimbali kutoa mchango wao wa mawazo na ikiwezekana kama kuna msaada tunaweza kupatiwa kwani tunapitia changamoto ya kukosa ajira serikali na hata kwenye sekta binafsi kwani tunakosa sifa kutokana na kukosa vyeti.
Asante.
UFAFANUZI WA NACTVET
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko wa Baraza la Taifa la Elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi (NACTVET), Jeff Shellembi anafafanua:
Mawasiliano baina ya Chuo husika na NACTVET yalifanyika. Utaratibu wa vyeti vya wahusika unafanyika. Jambo hili litakamilika karibuni na wahusika watapewa vyeti vyao kwa utaratibu uliwekwa.