Chuo cha Mipango Dodoma

hanley jr

Senior Member
Joined
Feb 26, 2013
Posts
119
Reaction score
27
wadau nimeapply chuo cha mipango dodoma kozi ya ba in development economics lakini baada ya kumwambia mzazi wangu amesema chuo hiko ni kibaya bila kunipa sababu zozote na deadline imepita tayari.

Msaada kwa wanaokijua hiki chuo je ni kuzuri au magumashi maana nimechanganyikiwa tayari naombeni msaada wa maoni yenu, asanteni mbarikiwe.
 
Du basi mzee hakijui chuo hicho, uliza waliomaliza pale wangapi wapo mtaa kwa ngazi ya shahada?

Halafu kozi yenyewe hiyo chuo gani kinatoa zaidi ya mipango? Zingatia neno Development Economics ujue huo ni uchumi unaotafsiri maisha ya watu unaenda kudeal na paretmeter za development!

Nenda hutajilaumu mimi nimesoma post graduate pale sijilaumu!! Ila jiandae kuna mchaka mchaka, kuishi porini field nyingi za kulala kwenye matent na kuandaa documents sectoral plans, integrated plans etc, lazima ujiandae spss kuielewa kwaajili ya analysis takwimu na research pale ndo nyumbani!

Haya safari njema.
 
ubaya wake ni umalaya ila usiogope hii ni kwa vyuo vyote bongo!
 
Ni chuo kizuri sana ila jipange kwani mziki wa pale si mchezo, kuna prof anaitwa Ziliona nomaa, babu ndile balaha, kudisco jambo la kawaida.

Mke wa waziri mmoja alidisko palepale, jipange ka. Mimi nimesoma pale masters ya economics, chuo kizuri sana.
 
Kile chuo ni cha tofaut sana. Coz zake hazipatikani kwingine. Nimesoma pale coz ya regional development planning, japokuwa sijapata ajira bado Larkin sijutii kusoma pale.

Lakin ukienda pale nenda ukiwa umejiandaa kusoma maana pale mchaka mchaka kama alivosema mdau hapo juu.

Kuhusu ubaya wa chuo muulize vizuri huyo mzazi wako labda anajua ubaya wake. Vinginevyo chuo ni kizuri.
 
Me nimesoma udom ila pale mipango kupo fresh kabisa coz kile chuo kina coz unique uyo mzazi wako anadegree?

Kweli wazazi wengine majanga ila mweshimu tu maana ndo mzazi,ila Vijana muwe muna maamuzi yenu binafsi coz maisha ni yako mzazi anayo nafasi ndogo sana katika maisha yako hasa umri wako unavyozidi kuwa.

Jiulize, je mbona kuna watu hawana wazazi ila maisha yao yapo kwenye njia sahihi?
 
Huyo mzazi wako anataka usomee nini? nenda mafunzo ya mgambo ili uwe mlinzi basi! Hicho chuo ni kizuri!
 
kuna kozi nyingine pale ya development finance and investment planning nasikia ni nzuri sana na ya kipekee
 
mimi piq ni mmojawapo ya walioomba mipango dodoma nimeomba development finance and investment planning ni pazuri
 
mimi piq ni mmojawapo ya walioomba mipango dodoma nimeomba development finance and investment planning ni pazuri

kweli kabisa mkuu hiyo kozi nimesoma course contents zake ni nzuri sanaaa haipatikani chuo kingine chochote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…