KWELI Chuo cha MUST kimetangaza fursa za masomo bure

KWELI Chuo cha MUST kimetangaza fursa za masomo bure

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Hii ni kweli??l
c8446027-7ab5-49ec-8012-2f1dca421c4d.jpeg
 
Tunachokijua
Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Mbeya (MUST) ni matokeo ya mabadiliko kutoka Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Mbeya (MIST) kupitia Sheria ya Vyuo Vikuu Na. 7 (2005) na Katiba ya Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Mbeya ya mwaka 2013.

Sheria ya Vyuo Vikuu inazitaka taasisi za elimu ya juu kuandaa katiba na kuzipitisha kama sharti la kutoa elimu ya chuo kikuu. Kwa kuzingatia matakwa ya Sheria ya Vyuo Vikuu, Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Mbeya kimeanzishwa chini ya Sehemu ya II, Kifungu cha 3(1) cha Katiba ya Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Mbeya ya mwaka 2013.

Kumekuwapo na barua inayosambaa mtandaoni ikidaiwa kutolewa na Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Mbeya ikiwa na taarifa ya uwepo wa nafasi za mafunzo ya ufundi stadi katika chuo hicho yanayofadhiliwa na serikali kwa asilimia 100%


Je, uhalisia wa barua hiyo ni upi?

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck ulibaini kuwa taarifa kuhusu uwepo wa nafasi za mafunzo ya ufundi stadi katika fani mbalimbali ni ya kweli ambapo Wizara inayosimamia masuala ya Kazi, Maendeleo ya Vijana, Ajira na Ukuzaji Ujuzi pamoja na Ustawi wa Watu wenye Ulemavu ilichapisha kupitia tovuti na kurasa zake za mitandao ya kijamii ambapo serikali itafadhili ada ya mafunzo kwa 100%

Aidha Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Mbeya (MUST) ni moja kati ya vyuo vilivyoainishwa kwa ajili ya kutoa mafunzo hayo, huku JamiiCheck ikibaini kuwa barua iliyosambaa mtandaoni kuhusu chuo hicho kutangaza nafasi hizo za mafunzo ni halisi ambapo afisa udahili wa MUST Amani Simbeye aliithibitisha akisema maelezo yaliyopo kwenye tangazo yapo sahihi, wanaohitaji wafuate maelekezo kama yalivyo ili kupata fursa hiyo.

"Ni sahihi, tangazo ni la kwetu, ni moja kati ya program zilizopo chini ya Ofisi za Waziri Mkuu, hivyo ni kweli hayo maelezo yaliyopo kwenye tangazo yapo sahihi, wanaohitaji wafuate maelekezo kama yalivyo." alisema Simbeye​
Back
Top Bottom