Down To Earth
JF-Expert Member
- Jul 8, 2011
- 21,940
- 16,643
Chuo cha taifa cha usafirishaji, ni moja kati ya vyuo vikongwe hapa TANZANIA ambavyo serikali ‘imeamua' kukipiga chini katika uboreshwaji wake!
Ndugu wadau, chuo cha taifa cha usafirishaji kinajivunia ‘ghorofa' ambalo mpaka sasa ujenzi wake unaenda kwa speed ya kinyonga aliyevunjwa miguu.. yaani, bila pesa za wanafunzi (ada) basi hili jengo haliendi. Sijui kama dr mwakyembe anafahamu lolote kuhusu jambo hili.
NIT imefanya enrollment ya wanafunzi zaidi ya 300 katika mwaka huu wa masomo 2013/2014 wakiwa na mategemeo kwamba, jingo hili linalojengwa lingekuwa tayari ili liweze kutumika katika masomo, lakini cha ajabu ni kwamba, mpaka chuo kinafunguliwa October mwishoni, hakuna kilichokuwa kimefanyika. Tafadhali dr mwakyembe, kama umefanikiwa kuuona huu uzi, wewe kama waziri wa uchukuzi, chukulia hili suala kiundani zaidi!
Ndugu wadau, kesho ni mahafali ya 29 ya chuo cha usafirishaji, kwa umri mkubwa wa chuo kama hiki, nilitegemea kwamba, kingekuwa angalau na sifa kama chuo kikuu cha dar es salaam (UDSM), hii iko wazi, na ingewezekana kabisa.
Pia, harakati zinazoendelea hivi sasa za chinichini hapa nit ni kuhusu ujenzi wa hostel zenye uwezo wa kulaza wanafunzi 1000. Sasa je, kwanini tender hii haitangazwi wazi ili wadau waichangamkie?? Je kuna ujanja mwingine ambao unataka kufanyika hapa?
Chuo hiki kina historia ndefu sana wadau.. HONGERA KWA DR MGANILWA KWA JUHUDI ZAKO ULIZOONYESHA NDANI YA MUDA MFUPI ULIOINGIA MADARAKANI!
Kama kuna swali lolote, please naomba kuulizwa!