Chuo cha taifa cha usafirishaji.. Moja kati ya vyuo vya kale vilivyosahauliwa na taifa!

Chuo cha taifa cha usafirishaji.. Moja kati ya vyuo vya kale vilivyosahauliwa na taifa!

Down To Earth

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2011
Posts
21,940
Reaction score
16,643
Chuo cha taifa cha usafirishaji, ni moja kati ya vyuo vikongwe hapa TANZANIA ambavyo serikali ‘imeamua' kukipiga chini katika uboreshwaji wake!

Ndugu wadau, chuo cha taifa cha usafirishaji kinajivunia ‘ghorofa' ambalo mpaka sasa ujenzi wake unaenda kwa speed ya kinyonga aliyevunjwa miguu.. yaani, bila pesa za wanafunzi (ada) basi hili jengo haliendi. Sijui kama dr mwakyembe anafahamu lolote kuhusu jambo hili.

NIT imefanya enrollment ya wanafunzi zaidi ya 300 katika mwaka huu wa masomo 2013/2014 wakiwa na mategemeo kwamba, jingo hili linalojengwa lingekuwa tayari ili liweze kutumika katika masomo, lakini cha ajabu ni kwamba, mpaka chuo kinafunguliwa October mwishoni, hakuna kilichokuwa kimefanyika. Tafadhali dr mwakyembe, kama umefanikiwa kuuona huu uzi, wewe kama waziri wa uchukuzi, chukulia hili suala kiundani zaidi!

Ndugu wadau, kesho ni mahafali ya 29 ya chuo cha usafirishaji, kwa umri mkubwa wa chuo kama hiki, nilitegemea kwamba, kingekuwa angalau na sifa kama chuo kikuu cha dar es salaam (UDSM), hii iko wazi, na ingewezekana kabisa.

Pia, harakati zinazoendelea hivi sasa za chinichini hapa nit ni kuhusu ujenzi wa hostel zenye uwezo wa kulaza wanafunzi 1000. Sasa je, kwanini tender hii haitangazwi wazi ili wadau waichangamkie?? Je kuna ujanja mwingine ambao unataka kufanyika hapa?

Chuo hiki kina historia ndefu sana wadau.. HONGERA KWA DR MGANILWA KWA JUHUDI ZAKO ULIZOONYESHA NDANI YA MUDA MFUPI ULIOINGIA MADARAKANI!

Kama kuna swali lolote, please naomba kuulizwa!
 
Ndugu wadau, nimezungumzia kwa uchache sana kuhusu suala la accomodation. ukweli ni kwamba, kwa jinsi wadau wanavyosema hapa (kutoka kwa wanafunzi wa miaka ya juu) ni kwamba, mkuu wa chuo aliyepita, before dr mganilwa, NSSF walikuja hapa na kutaka kufanya investment katika malazi. lakini cha ajbu ni kwamba mkuu yule aliyekuwa madarakani, alikataa katakata kuhusu huo mradi!!!

sasa madhara yake ndio yanakuja kuonekana sasa, wanafunzi wamechaguliwa wengi mno kwa mwaka huu wa masomo!!! sehemu za malazi ni chache sana na zilizopo haziwezi tosheleza wanafunzi hawa, na istoshe, si NIT pekee iliyoko hapa, kna vyuo vingine vingi ikiwemo IFM, UDSM na wengineo ambao wanahitaji malazi!

kwa hiyo, demand imekuwa kubwa sana kuliko supply hivyo imepelekea kwa wenye hostel kupandisha bei ovyo ovyo bila sababu maalumu!
 
vp kuhusu suala la sehemu ya chakula, sio siri mimi nipo first year ila sielewi mpka mda huu nn knaendelea kwny suala hilo mana 2nahangaika kuvuka barabara kitu ambacho kinaweza sababsha ajal wkt wa kuvuka road..
 
Mmmhhh mbona NIT wameshinda tender ya ukaguzi WA magari! Na kwamba ule mchezo WA kukagua magari nje ya nchi utafikia mwisho very soon.

PIA wanaanzisha kozi mpya inayohusiana na masuala ya ndege ambayo Itakua unique kote East and central Africa.
 
Tatizo wanafunzi WA pale baadhi Yao ni wezi WA chakula kama wake wanaoibaga chips mayai pale Muleba Bar. Aibu kweli
 
Naamnini waziri na wizara yenye dhamana husika watakua wameskia hivi vilio
 
Mpwa wangu nimekutaka radhi japo ukweli unabaki kuwa ukweli, i was there ndio maana, sijatunga, nilikuepo siku ya tukio kiongozi

kwamba ulikuwepo wakati chips zinaibiwa? na wanafunzi wakatoa vitambulisho kwamba ni wa nit? ama uliwatambuaje?

dah, huu ni upakaziaji wa hali ya juu!
 
Elli wherever you are come here and answer the arguement....!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Excel huyu dr mganilwa kanipigisha pindi la eng. Design jamaa yuko njema asee!!! Na kweli ni mtu wa kazi!!
 
Last edited by a moderator:
Ndugu wadau, nimezungumzia kwa uchache sana kuhusu suala la accomodation. ukweli ni kwamba, kwa jinsi wadau wanavyosema hapa (kutoka kwa wanafunzi wa miaka ya juu) ni kwamba, mkuu wa chuo aliyepita, before dr mganilwa, NSSF walikuja hapa na kutaka kufanya investment katika malazi. lakini cha ajbu ni kwamba mkuu yule aliyekuwa madarakani, alikataa katakata kuhusu huo mradi!!!

sasa madhara yake ndio yanakuja kuonekana sasa, wanafunzi wamechaguliwa wengi mno kwa mwaka huu wa masomo!!! sehemu za malazi ni chache sana na zilizopo haziwezi tosheleza wanafunzi hawa, na istoshe, si NIT pekee iliyoko hapa, kna vyuo vingine vingi ikiwemo IFM, UDSM na wengineo ambao wanahitaji malazi!

kwa hiyo, demand imekuwa kubwa sana kuliko supply hivyo imepelekea kwa wenye hostel kupandisha bei ovyo ovyo bila sababu maalumu!
hili suala pia lipo hata mzumbe,ardhi ,ifm,udsm,na vyuo vingine.selikali hata kama imevipa nguvu ya kujitegemea basi iwe inatoa hata rudhuku.pia makosa si ya wakuu wa chuo,mfano mzumbe waliweka mpaka harambee ya kujenga mabweni ,pia mpaka ikawa inawaomba watu wawekeze kule.tatizo lingine pia ni kwamba hela inayochajiwa kwa wanafunzi wanaotumia hostel ni ndogo(SHILINGI MIA TANO.500/- KWA SIKU)HII INASABABISHA VYUO VYA GOVERMENT KUSHINDWA KUJENGA MABWENI KUTOKANA NA KODI WANAYOWACHAJI WANAFUNZI
 
Back
Top Bottom