Chuo cha ualimu Kinampanda-Iramba Singida hatarin kuwapoteza mkuu wa Chuo na Makamu wake

mapambanodaima

Senior Member
Joined
Oct 22, 2012
Posts
108
Reaction score
15
Ndugu wanabodi kuna taarifa zimenifikia muda si mrefu kuwa inawezekana kabisa mkuu na makamu wake kuondolewa chuon kwa kile kinachosemekana utendaji mbovu na ufisadi.

Wanachuo waligoma wiki iliyopita baada ya kupewa vifaa vya kufundishia visivyozidi thamani ya sh.2000 wakati walipaswa kupewa 33000.

Naibu waziri wa elimu,mkurugenzi wa mafunzo ya ualimu,DC uongozi wa elimu wa wilaya na Bodi ya chuo wapo kwenye kikao na wanachuo,na baada ya hapo watazungumza na wafanyakazi wa chuo. Nitawapa update kadiri nitakavyokuwa napata taarifa. Source aliyopo kwenye eneo la chuo.
 
Dah umenkumbusha Tumaini sec shule yangu!
 
Kuna uozo wa kutisha hapo chuoni. Nilifanya visit hapo mwaka jana na nilijionea namna principal na vice wake walivyoigeuza hiyo taasisi na kuwa kama mali yao. They should be fired.
 
Asante sana mkuu kwa taarifa.Taasisi zetu hizi zina matatizo mengi sana dawa ni kuondoa system zote mbovu,kama ilivyofanyika kwa chuo cha ualimu korogwe kwa kumvua ukuu bwana Mwiga na makamu wake na baadhi ya wakufunzi kuhamishwa chuoni hapo.Mapambano yanaendelea
 
Eee bana unanikumbusha mbali....enzi za Mangw'enyengw'enye (Mr.Shilla) akiwa ndio Head Master - Namkumbuka mwenyekiti wa shule wakati huo (1982 - 1985) - James Midigo ( Cheyo) na kundi lake - Lotah, Colourless, Jomba, na......shule ilikuwa balaa miaka hiyo, Sasa nasikia ni GIRLS SEC SCHOOL
 
Tunaomba utupe update ya kile kinachoendelea maana ni chuo nilichosoma mwaka 2008 Mkuu wa chuo akiwa R.MAGUBIKI na Makamu akiwa MPONDO nidhamu MAMA MANSILLO Wenga,Sebastian wako poa sana marafiki zangu!
 
KYALOSANGI jina la shule ya msingi taja jina lako ntakufahamu kwani ni mwenyeji sana isitoshe nilikuja mwaka jana tu kuijia cheti changu cha ualimu.
 

updates. Tayari mkuu wa chuo Thesia Kivanda na makamu Imael Mpondo wamevuliwa madaraka na mkuu wa chuo kutakiwa kupeleka bank statements za miaka 2 na matumizi fedha kwa akaunt binafsi aliyofungua kwa ajili ya kulipia michango tofauti na ada
 

daaa mmenikumbusha mbali yule maza alinifanya nikaruka ghorofani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…