Chuo cha Udereva.

Double N

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2018
Posts
290
Reaction score
550
Kwema ndgu zangu...
Ni ndgu yenu Mmanyanigho hapa, nilipost thread ya kuja dar
Sina namna nakuja Dar

Sasa Dar nilifika salama, nimehustle mpaka nimepanga chumba maeneo ya uswahilini kidogo ila naishi kibingwa.

Hii thread ya leo naomba kujuzwa vyuo vinavyotoa mafunzo ya udereva hasa evening classes maana nna kibarua kinachoniweka mjini hivyo jioni ndio nina muda.

Na pia jinsi ya kupata leseni ya udereva, dili nyingi zinanipita kwa kukosa leseni ya udereva.

Natanguliza shukran zangu za dhati yeyote atakaenisaidia kwa lolote.
 
Kuna chuo Mwenge hapo kinaitwa Victory ni wakongwe na unaweza chagua muda ambao kwako ni rafiki kwenda ikiwa ni asubuh sana au jioni shukia kituo kinaitwa Lufungila.

Kuhusu leseni ,Ukikamilisha mafunzo yako utaelekezwa vizuri kabisa hapo chuoni nini ufanye.
 
Vipi kuhusu gharama zao, una habari zozote kuhusu hilo?
 
Habari mkuu. Kwa kuwa wewe ni hustler napenda nikushauri kitu kimoja. Kama unajimudu basi nenda kajifunze udereva katika vyuo vya SERIKALI hasa VETA kwa sababu hicho chua kinaaminika sana kwa wanaohitaji kuajiri madereva hasa mashirika na taasisi za umma.

Kila la kheri
 
U
Ukipata chuo,hukohuko utapatiwa lesen.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…