CHUO CHA UNESI KINACHUKUA DiV-0?

CHUO CHA UNESI KINACHUKUA DiV-0?

Enny

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2009
Posts
962
Reaction score
130
mtoto wa jirani yangu amepata Div - 0, nimemsikia jirani yangu anasema huyu kafeli sasa inabidi nimpeleke chuo cha unesi huko mkoani. hapo nikajiuliza kuna chuo kinachukua Div -0?
 
hakuna kitu kama iko kama hadi bio kafeli sasa atajua kidonda..
 
Mimi shemeji yangu akapata Div IV ya point 29 ningependa sana aende huko huko kwenye Nursing kama atapokelewa. Mwenye kufahamu chuo naomba aniPM.
 
mtoto wa jirani yangu amepata Div - 0, nimemsikia jirani yangu anasema huyu kafeli sasa inabidi nimpeleke chuo cha unesi huko mkoani. hapo nikajiuliza kuna chuo kinachukua Div -0?

cannot find server!Check your internet connections!
 
Mimi shemeji yangu akapata Div IV ya point 29 ningependa sana aende huko huko kwenye Nursing kama atapokelewa. Mwenye kufahamu chuo naomba aniPM.

Kama amepata D's za Chemistry,Physics na Biology atapokelewa Nursing ngazi ya cheti,bila hivyo hakuna nafasi.
 
kama amepata d's za chemistry,physics na biology atapokelewa nursing ngazi ya cheti,bila hivyo hakuna nafasi.
mkuu application zao na ada zao zinaendaje hivi vyuo, ila akiwa na d tatu anaweza ngonga diploma
 
chuo kipo kinaitwa msimbazi center kipo ilala dar es salaam......kinachukua kuanzia la saba mpaka form four.....na kipo chini ya wizara
 
Acheni hizooo...division 0 kwenye unesi mtu anachukuliwa ila tuu awe na division 1 ya "witooooo"
 
chuo kipo kinaitwa msimbazi center kipo ilala dar es salaam......kinachukua kuanzia la saba mpaka form four.....na kipo chini ya wizara

Wanahitimu wa hapo wanaitwa Medical Attendants....tatizo letu kila tunayemuona wodini tunadhani ni Nurse! Angalia uniform zao mkuu, wanaovaa nyeupe na lebo hizi mabegani: EN,RN ndio hao wa Physic,Chemistry na Biology...tena sasa hivi kabla hawajafanya mitihani yao ya kumaliza vyuo,vyeti vyao vya kidato cha nne(orijino)vinatumwa wizarani kuhakikiwa kama ni feki au safi......mambo ni magumu kote kote,hata u-Polisi nasikia ni angalau uwe na D tatu za o-level.
 
Acheni hizooo...division 0 kwenye unesi mtu anachukuliwa ila tuu awe na division 1 ya "witooooo"

angalia tangazo uliposoma ni la mwaka gani,...hiyo division kama inamfanya nurse afahamu kutofautisha vein na artery ili aweze kuweka drip,au ku-calculate uzito wa mwili wa mgonjwa ulingane na idadi ya vidonge vya 'piriton' hapo nakubaliana na wewe....
 
mkuu application zao na ada zao zinaendaje hivi vyuo, ila akiwa na d tatu anaweza ngonga diploma

Nina uhakika na chuo kinaitwa Rubya School of Nursing kipo karibu na Muleba mjini,kinatoa mafunzo ya Nursing ngazi ya diploma. Masharti ni lazima uwe na angalau D za Biology,Chemistry,Physics/Math na English. Pia lazima upass entrance exams. Ada ni kama 1mil.kwa mwaka, maombi hutumwa pale kuanzia Feb. Anwani:
Principal,
Rubya School of Nursing,
P.O.Box 133,
RUBYA.
BUKOBA.
 
Mimi shemeji yangu akapata Div IV ya point 29 ningependa sana aende huko huko kwenye Nursing kama atapokelewa. Mwenye kufahamu chuo naomba aniPM.

chamsingi awe amepata Daraja 'D' ya Biolojia basi hakuna zaidi! Mpeleke akapambane!
 
Mwenyewe Jirani yangu kapata FLD 34 ana 'D' ya kiswahili hadi saivi anafuatilia barua kutoka serikali za mtaa ili aweze kwenda chuo 'Ati kapata chuo cha Nursing?' teh teh teh teh, Taifa laangamia kwa kukosa Maarifa!
 
mtoto wa jirani yangu amepata Div - 0, nimemsikia jirani yangu anasema huyu kafeli sasa inabidi nimpeleke chuo cha unesi huko mkoani. hapo nikajiuliza kuna chuo kinachukua Div -0?

hahaaa kipo mtwara...si ndo hao wanachoma potassium permanganate wagonjwa
 
Back
Top Bottom