Mwita Maranya
JF-Expert Member
- Jul 1, 2008
- 10,565
- 7,984
Najua kuna Utofauti ila kwa upande wangu naona ni mdogo sana hadi ziwe kozi mbili tofauti..Sidhani ka mtu aliyesoma Procurenent & logistics mgt atashindwa kufanya kazi za mtu wa Logistics & Transport mgt
Mkuu yani unataka tukuamini kwamba hakuna tofauti kubwa kiasi hicho, kwamba huoni ama hukubali kwamba transport na procurement ni vitu viwili tofauti?
Tuliza akili yako kidogo utaona utofauti wa "Logistics and transport management" vs "procurement and logistics management", au nikikuuliza usafirishaji na ununuzi ni kitu kimoja? ama kinachokupa tabu ni hiyo logistics kuingia pande zote?
Kufanya kazi ambayo hujasomea ni kitu kimoja na kufanya kazi kwa ufanisi ni kitu kingine, na hili ndilo tatizo la watu wengi kupenda short cut, kila mtu anatakiwa afanye kazi ya taaluma yake, tuache ujanja ujanja huu hautusaidii sana kama taifa. Haya ndio maajabu ya mtoto wa makamba kasoma political science halafu amepewa nafasi ya kuwa mkurugenzi wa masoko katika kampuni ya simu!!