Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Salaam,
Baada ya Mdau wa JamiiForums kulalamikia Ratiba ya Masomo ya Chuo cha ustawi wa jamii Kwamba Wanafunzi wanasoma hadi hadi saa 4 usiku kitu ambacho ni hatari kwa usalama wa wanafunzi, Chuo kimetoa Ufafanuzi.
Katia taarifa yao wameeleza hivi;
Tarehe 3 Novemba, 2024 ilisambaa taarifa katika mitandao ya kijamii yenye kichwa cha habari "Ratiba ya Masomo hadi saa 4 usiku Chuo cha ustawi wa jamii ni hatari kwa usalama wa wanafunzi".
Tunapenda kutoa ufafanuzi wa jambo hilo kwamba, upangaji wa ratiba ya masomo katika Chuo cha Ustawi wa Jamii unafanyika kwa kuangalia vigezo mbalimbali kama vile idadi ya wanafunzi katika programu husika na ukubwa wa vyumba vya mihadhara. Kutokana na idadi ya wanafunzi kuongezeka mwaka hadi mwaka, programu zenye wanafunzi wengi hulazimika kugawanywa katika makundi mawili au zaidi ili waweze kutosha katika vyumba vya mihadhara vilivyopo.
Katika mgawanyo huo wa makundi, baadhi ya wanafunzi huanza vipindi vyao mapema saa moja asubuhi na kumaliza wakati wa mchana. Makundi mengine huanza vipindi wakati wa mchana na kumaliza kati ya saa 12 jioni na saa nne usiku. Aidha, ieleweke kwamba mwanafunzi yeyote anakuwa huru kuchagua kuwa kwenye kundi la wale wanaoanza vipindi mapema asubuhi au wale wanaoanza vipindi vyao baadae mchana.
Kwa hiyo katika muktadha huo, kusoma vipindi vinavyoanza asubuhi au mchana ni uchaguzi wa mwanafunzi mwenyewe na Chuo kimekuwa na utaratibu wa kuwashirikisha wanafunzi kila rasimu ya ratiba ya masomo inayoandaliwa. Vilevile kwa wanafunzi wanaoishi mbali na eneo la Chuo, wamekuwa wakishauriwa kutafuta makazi karibu na Chuo ili waweze kuhudhuria vipindi mbalimbali vya masomo yao kwa ufanisi.
Hivyo, tunapenda kuujulisha Umma kwamba taarifa iliyotolewa ni ya upotoshaji na haina mantiki kwa vile utaratibu huu umekuwa ukifuatwa na vyuo mbalimbali hapa nchini.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano na Masoko