Synonyms MP
JF-Expert Member
- Jun 4, 2024
- 320
- 346
Haya aongeze mbinu na TTCL iende PPPView attachment 3101816
Chuo kikuu Cha Usimamizi wa Fedha na Biashara Cha CBE nchi Tanzania kimemtunuku Mhe David Kafulila ngao ya heshima kwa uchapakazi wake uliotukuka kwa Taifa.
Mkuu wa Chuo hicho Prof Edna Luoga asema Chuo hicho kimeamua kutoa ngao hiyo ya kutambua juhudi za Kafulila katika kumpata mwekezaji atakayejenga mabweni katika Chuo hicho yatakayoweza kuchukua wanafunzi elfu 12 kwa mara moja kwa sharti la Ubia ili kukabiliana na tatizo la wanafunzi kuishi mbali na eneo la Chuo hicho jambo ambalo hupunguza ari na nguvu za Masomo kwa wanafunzi hao.
David Kafulila ambae ni Mkurugenzi mkuu wa Ubia kati ya Serikali na Sekta binafsi Tanzania PPP amekuwa akisistiza lazima ifike mahali ambapo Serikali ipunguziwe mzigo katika Utekelezaji wa miradi ya maendeleo hasa miradi yenye sura ya kibiashara ili kuifanya Serikali itekeleze baadhi ya miradi yake ya maendeleo nje ya bajeti yake ( Outside the government balance sheet)