View attachment 3101816
===
Chuo Cha Usimamizi wa Fedha na Biashara Cha CBE nchi Tanzania kimemtunuku Mhe David Zacharia Kafulila ngao ya heshima kwa uchapakazi wake uliotukuka kwa Taifa lake.
Mkuu wa chuo hicho Prof. Eddnah Luoga asema chuo chake kimeamua kumtunuku ngao hiyo ya heshima katika kutambua juhudi zake kwenye kumpata mbia mwekezaji toka sekta binafsi atakayejenga mabweni katika chuo hicho yatakatokuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi elfu 12 kwa mara moja.
Mwekezaji huyo atawekeza kwa sharti la Ubia ili kukabiliana na changamoto za wanafunzi kuishi mbali na eneo la chuo hicho jambo ambalo hupunguza zaidi ari, ufaulu na nguvu za kimasomo kwa wanafunzi.
David Zacharia Kafulila Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Ubia kati ya Serikali na Sekta binafsi Tanzania PPPC amekuwa akisisitiza wakati wote kuwa lazima Tanzània ifike wakati ambao Serikali yetu itapunguziwa mzigo katika kutekeleza miradi yake ya maendeleo hasa ile yenye sura ya kibiashara.
Mkurugenzi huyo anasema kwa kufanya hivyo kutaipunguzia Serikali mzigo na kuifanya itekeleze baadhi ya miradi yake ya maendeleo nje ya bajeti yake hasa ile yenye sura ya kibiashara ( projects contraction outside the government balance sheet )
===
View attachment 3104529