gcmmedia
Member
- Jul 19, 2024
- 49
- 96
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kinawanyonya na ninahisi kimejengewa mfumo usio rasmi wa kuwaibia vijana wanawabakisha mara baada ya kuhitimu masomo kwa ufaulu mzuri ili kusaidia kusimamiw semina na kufundisha (tutorial assistants).
Vijana hawa kwa muhula wa pili sasa mwaka huu hawajalipwa malipo yoyote. Wazazi wanawagharimia nauli, chakula na malazi, kana kwamba ni wanafunzi.
Inapokaribia mwisho wa semister, chuo huwaletea mikataba ya kazi hiyo iliyokosewa na kuirudisha kurekebisha. Ikirekebishwa na kusainiwa, huipeleka na kukaa nayo kimya, hawawalipi wala kuwapw nakala ya mikataba ya kazi hizo.
Kibaya zaidi, baadhi ya vijana hao wanaopata ajira kwingine huondoka bila malipo yao (na huu unakuwa mwisho). Swali: Je, malipo yao huenda wapi? (Hapa ndipo nina wasiwasi mfumo wa kuwaibia vijana hawa unakuwa, nina wasiwasi kuna watu wananufaika na hili).
Inaonekana hii imekuwa ikifanyika kwa makusudi miaka ya hivi karibuni mara kwa mara.
Vijana hao hawana wa kumlilia kwani wasimamizi wao na idara zao huwapiga chenga tu bila majibu ya malipo yao. Wanaishi kwa kutumaini ipo siku watalipwa au watapata ajira ya kudumu. Hii maana yake Chuo kinatumia tatizo la kukosa ajira kujinufaisha na ama kuwanyonya vijana au baadhi ya naafisa wake huchelewesha malipo ili wabaki nayo.
Kwa taasisi kubwa na ya kitaaluma kama UDSM jambo hili ni la aibu na fedheha kubwa sana.
“A University is a center of excellency”. Kamwe hawapaswi kufanya mambo haya ya aibu. Chuo kiache kunyonya vijana, kiwalipe malipo yao stahiki kwa majukumu ambayo wanayatekeleza.