Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kuandaa sera za matumizi ya Akili Mnemba (AI) kwa maendeleo ya elimu nchini

Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kuandaa sera za matumizi ya Akili Mnemba (AI) kwa maendeleo ya elimu nchini

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kimeanza kutengeneza sera na miongozo ya matumizi ya teknolojia ya akili mnemba ili kuhakikisha teknolojia hiyo inatumika kwa faida.

Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Lugano Kusiluka, amesema hayo leo Jumatano, Desemba 4, 2024, wakati wa kongamano la 15 la wanazuoni.

“Kwenye vyuo vikuu bado kuna majadiliano kuhusu faida na hasara yake, lakini hoja ni tunaitumiaje ili iweze kuleta faida,” amesema.

Amebainisha kuwa akili mnemba ni teknolojia inayotumika sana duniani, hivyo haiwezi kupuuzwa. “Tunapaswa kuangalia jinsi ya kutumia teknolojia hii kuboresha taaluma na kazi za wanafunzi,” amesema Profesa Kusiluka.

Ameeleza changamoto kubwa kuwa ni kutambua kama kazi zilizowasilishwa ni halisi au zimetokana na akili mnemba. Hivi sasa UDOM ina wataalamu na miradi inayotumia teknolojia hiyo, huku ikiendelea kutengeneza miongozo inayoendana na mazingira ya Tanzania.

 
Back
Top Bottom