Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba cha Bugando: Hatubadili vigezo vya ufaulu

safi sana bugando. endeleeni kukaza. naona hii nchi huko tunakoelekea hata ukiwa na apgar score ya mbili utaweza kwenda medical school
 
Kwakweli kulegeza viwango vya ufaulu kwa madaktari ni kutaka kutuangamiza. Hili ni suala la maisha ya watu na afya zao.
 
safi sana mi nawapongeza huu ni uwendawazimu kufaulisha wanafunzi ambao hawana uwezo na vyuo vingine viige
 
Hii ni siasa tu za kujifanyia marketing tu.Mbona wapo wengi wamepitia hapo na ni vilaza tu huku makazini?Hata huo mfumo wenu wa kutambua ufaulu wa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga hapo naona kama haufanyi kazi vizuri kwani kuna watu walighushi vyeti na wakasoma hapo wakamaliza vizuri tu.Halafu hao wanaoshindwa kufikia vigezo mnawashauri wakasome fani gani zinazopokea vilaza?Badala ya kumchuja mtu kabla hajaanza kusoma,wapeni nafasi na wachujwe na CA iwapo hawana uwezo.Mimi ninamfahamu mtoto mmoja amesoma st Kayumba,walimu wanne tu shule nzima lakini akafaulu div III licha ya changamoto nyingi za ufukara wa kwao. Anauwezo mkubwa sana akipata nafasi hata hapo kwenu mtamshangaa.Semeni mnavyotenda na tendeni mnavyosema.Acheni siasa.

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Halafu hii fani ya udaktari msitake kuwatisha sana watu kana kwamba ni kitu cha pekee sana kwa wateule wachache mno wenye akili zisizo za kawaida(nyingi?!)HAPANA!Ni fani ya kawaida na mtu yeyote mwenye wito(huhitaji AA tu)anaweza akasoma vizuri na akawa daktari mzuri sana.Mifano iko mingi mno.Wako baadhi ya watu wengi darasa la saba tu wamekuwa wakiwasaidia specialists wazungu wanaokuja kufanya kazi hospitali za mission(bahati nzuri wazungu hufundisha maarifa si wachoyo)wamefanikiwa kufanya surgical operation ngumu ingawa madaktari hili hawawezi kukiri.Sisemi kila mtu anaweza kuwa daktari,La!bali ni kama ambavyo si kila mtu anaweza kuwa mwanamuziki,ndivyo na udaktari pia.Maarifa yanapokeleka vizuri tu.Si vema kuwatisha watu eti fani ya udaktari ni tofauti kwa upekee mkuubwa kiasi cha kwamba bila A mtu hawezi kusoma.Acheni usomi wa kizamani kwani kila binadamu ana uwezo mkubwa sana ambao hajautumia aidha kutokana na mazingira,makuzi na mambo aliyoaminishwa.

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Kuna jamaa 'wanaendesha" chuo fulani cha kupewa sijui watakuwa na msimamo gani kuhusu hii hali.
 

Mkuu upo sawa kabisa, hao jamaa wamejaza vilaza hapo kupitia zile programs zao za pre entry ambapo hata wenye div. Four wameweza kujiunga na school of medicine.
 

Salute mkuu, nimependa maneno yako...absolute truth!
 

Very nice comment,wamchukue tu mtu kama kilaza basi course itamshinda,ila kuwakatisha tamaa mapema sio mpango
 
Safi sana.....
Lakini CCM kwa jinsi walivyo na husuda na hiana hawachelewi kuwapoteza wakuu wa chuo hiki na kukifungia kabisaaaa
 

Umenena Mkuu !!
 

udaktari sio kukata tu,ngoja nikuambie watu wanamna iyo wanafanya kazi kwa mazoea tu, mfano anaweza fanya upasuaji wa mgojwa wa appendix leo bila shida yoyote ile, kesho anakuja mgonjwa mwingine tena mwenye appendix lakin blood pressure=200/110, mheshiwa std 7 atajidai tena kufanya operation tena kwa kujiamini,kitakachofuata kuandaa manzishi kwa marehemu.
 

tz huwezi fanikiwa bila kuwa mwongo na mnafiki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…