Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,107
- 160,001
CHUO KIKUU CHA DODOMA KUNA NINI?
Tumepokea malalamiko kutoka kwa wanafunzi kadhaa walio tarajiwa kuhitimu masomo yao kati ya mwaka2023/2024 kwamba zaidi ya wanafunzi 400 wamekuwa Discontinued kwa tuhuma za Jumlà.
Msingi wa Malalamiko ni Kwamba Uongozi wa Chuo uliwaambia wanafunzi hawa kwamba wameingilia mfumo wa Matokeo wa Chuo na Kubadilisha matokeo yao.
Wakimaanisha kwenye mfumo wa matokeo wa UDOM SR2
Na kwamba baada ya tuhuma hizi ambazo wanadai hazikuwa na uthibitisho wali zuiliwa kufanya graduation mwaka 2023 badala yake wakakamatwa na kupelekwa polisi.
Kwamba Polisi walichukua simu zao ili wakafanye uchunguzi na kwamba wamekaa mwaka mzima bila kupewa taarifa yeyote wala kujua uchunguzi uliishia vipi.
Kwamba mnamo mapema mwezi January 2025 wanafunzi hawa wali itwa Kituo Cha Polisi kutoa maelezo na kwamba mpaka sasa hawajawahi kupewa taarifa ya nini Polisi waliona kwenye simu zao ili waweze kujitetea au kutoa utetezi wao kwa ufasaha.
Kwamba katika Hali ya kushangaza wanafunzi hawa wote (400) wakaona kwenye mfumo wao wa Chuo kwamba wamekuwa Discontinued.
Wanafunzi hawa wanalalamika kwamba wamefanya jitihada za kuuliza Uongozi wa Chuo kuhusu haki yao ya kusikilizwa au haki ya rufaa na kwamba wamejibiwa wakate rufaa kwa Seneti ya Chuo.
Kwamba walipokwenda kwa ajili ya kufanya Utaratibu wa rufaa kwa Seneti kama walivyo elekezwa, seneti wamesema muda wa rufaa umeisha hivyo hawana muda wa kuendelea kupokea wala kusikiliza rufaa.
Aidha wanafunzi hawa wanalalamika kwamba kwa mfumo ulivyo hawakuwa namna ya kuingilia mfumo wa matokeo na kuubadili kama wanavgo singiziwa na uongozi wa CHUO
NI RAI YETU KWAMBA
1.Chuo Kikuu cha Dodoma ni Taasisi ya Umma ambayo inaongozwa kwa Mujibu wa Sheria na Kanuni ikiwamo maadili ya utumishi wa Umma na kwa msingi huo pia wanalazimika wakati wote kuzingatia matakwa na Masharti ya Sheria na Katiba ya Nchi.
2.Kwamba kwa hadhi ya Chuo hiki ni dhahiri kwamba wanatambua Msingi Mkuu wa Kikatiba kama unavyo onekana kwenye Ibara ya 9(a),(f) ,(h) ikisomwa pamoja na Ibara ya 13(6)(a) ya Katiba ya J̌amuhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu msingi wa kuzingatiwa wakati wa ufanyaji wà Maamuzi.
3.Kwambà haķi ya kusikilizwa ni pamoja na haki ya kujua kwa ufasaha tuhuma zinazokukabili mhusika na aina na asili ya tuhuma hizo ili aweze kuzijibu kwa ufanisi na kwamba Haki ya Kusikilizwa kwa haki inajumuisha haki ya kukata rufaa na kupewa uamuzi uliotolewa dhidi yako na sababu za uamuzi huo ili kukuwezesha kukata rufaa
4.Kwamba Seneti kukataa kupokea rufaa kwa sababu za jumla kwamba muda wa rufaa umekwisha bila kuzingatia muda ambao wa hanga hawa wamejulishwà kuhusu hatua na Maamuzi ya Chuo dhidi yao ni grave Injustice.
Tunatoa wito kwa Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dodoma kuchukua hatua za haraka kurekebisha na kulipatia ufumbuzi wa Haki tatizo hili ili kuzuia masuala ya Kitaaluma au shahada za Kitaaluma kwenda kutunukiwa Mahakamani.
CHUO CHA UMMA KINA WAJIBU MKUBWA ZAIDI WA KUULINDA UMMA na kuzingatia sana Maslahi mapana ya Umma na Misingi ya Haki wakati wote ili kujenga na kudumisha Maadili katika Utumishi wa Umma.
NI HATARI SANA KUPUUZA KADHIA YA WANAFUNZI 400.
Pia soma ~ Chuo Kikuu cha Dodoma chatoa ufafanuzi wa madai ya Wanafunzi 400 kuondolewa masomoni