DOKEZO Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) Kuna Nini? Wanafunzi zaidi ya 400 wame disqualify

DOKEZO Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) Kuna Nini? Wanafunzi zaidi ya 400 wame disqualify

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mifumo yote inadukuliwa duniani acha kashifa binadamu alotengenez mfumo anauwezo wa kuuharibu sas huo mfumo hufanywa na roboti au mwanadamu umefikilia au umeropoka na ukae ujue huo mfumo mpka hapo umedukuliwa na vijana na taasisi lazima ikipandisha matokeo inakuwa na backup yake kama system ikiwa collapsed au ikishake wanatumia backup ku restore data zao.

Kingine ujue ukiingilia mfumo mtu wa cyber anajua mfumo umeingiliwa kwa maana updation mpya na modification mifumo imetengenezwa kwa security kubwa wengine huletawa taairifa umebadilisha kitu fulani hiyo humpa expert kugundua mabadiriko kwa haraka.
Vijana wengi wana ujuzi wa kuingilia mifumo ila hawana ujuzi wa kujilinda kujua nani kahack mfumo na device zipi zimetumika hapo lazim wakudake muingiliaji wa mfumo na utataja kila aina ya jina au namba ulotumia kufanya modification..

Tusitetee ujambazi kama huyo anapata nguvu za kubadir zero yake kuwa 80 je atashindwa kukuibia pesa zako ulizimkabizi au kukwapua mali ya umma
Uko sahihi ila niamin mm wanafunzi wa UDOM wenye uwezo wa kuingilia SR2 ya UDOM katika 100 ni mmoja au hakuna kabisa....

Binafsi ikitokea mwanafunzi kafanikiwa kweli kuingilia mfumo basi huyo inabid aendelezwe na nchi ingawaje ni kosa ila hiyo ni potential lazima itunzwe kama wanavyofanya wenzetu.
 
Hii michezo inafanyika vyuo vikuu vingi hapa Tz, na wahusika wakuu ni ma IT wa vyuo husika. Sasa madogo wameliwa pesa na ITs alafu kimewalamba
 
Mbona hiyo rahisi tu
Kwani kila department si ina matokeo halisi ambayo wakufunzi wamepost kwenye mfumo; walinganishe tu kama kweli ni tofauti......Naamini wameshafanya hilo....
Tatizo naloweza kuliona ni kama waliobadili wamebadilisha na matokeo ya wengine ili kupoteza ushahidi...
Naamini Chuo pia kimejua kuwa ulinzi katika mifumo yake ya kimtandao inatakiwa kuimarishwa zaidi...
 
Uko sahihi ila niamin mm wanafunzi wa UDOM wenye uwezo wa kuingilia SR2 ya UDOM katika 100 ni mmoja au hakuna kabisa....

Binafsi ikitokea mwanafunzi kafanikiwa kweli kuingilia mfumo basi huyo inabid aendelezwe na nchi ingawaje ni kosa ila hiyo ni potential lazima itunzwe kama wanavyofanya wenzetu.
Yah hapo sikupingi katika kaka ila swala la kufanya modification ni kosa kubwa sana kisheria sijui kama hakufikilia ilo ila akiingia tu kutokufanya chochote huwaga hawana shida kabisa umeiva lakin imagine anapokea pesa za vijana alafu anabadili matokeo ni mambo ya kishenzi kabisa
 
CHUO KIKUU CHA DODOMA KUNA NINI?

Tumepokea malalamiko kutoka kwa wanafunzi kadhaa walio tarajiwa kuhitimu masomo yao kati ya mwaka2023/2024 kwamba zaidi ya wanafunzi 400 wamekuwa Discontinued kwa tuhuma za Jumlà.

Msingi wa Malalamiko ni Kwamba Uongozi wa Chuo uliwaambia wanafunzi hawa kwamba wameingilia mfumo wa Matokeo wa Chuo na Kubadilisha matokeo yao.

Wakimaanisha kwenye mfumo wa matokeo wa UDOM SR2

Na kwamba baada ya tuhuma hizi ambazo wanadai hazikuwa na uthibitisho wali zuiliwa kufanya graduation mwaka 2023 badala yake wakakamatwa na kupelekwa polisi.

Kwamba Polisi walichukua simu zao ili wakafanye uchunguzi na kwamba wamekaa mwaka mzima bila kupewa taarifa yeyote wala kujua uchunguzi uliishia vipi.

Kwamba mnamo mapema mwezi January 2025 wanafunzi hawa wali itwa Kituo Cha Polisi kutoa maelezo na kwamba mpaka sasa hawajawahi kupewa taarifa ya nini Polisi waliona kwenye simu zao ili waweze kujitetea au kutoa utetezi wao kwa ufasaha.

Kwamba katika Hali ya kushangaza wanafunzi hawa wote (400) wakaona kwenye mfumo wao wa Chuo kwamba wamekuwa Discontinued.

Wanafunzi hawa wanalalamika kwamba wamefanya jitihada za kuuliza Uongozi wa Chuo kuhusu haki yao ya kusikilizwa au haki ya rufaa na kwamba wamejibiwa wakate rufaa kwa Seneti ya Chuo.

Kwamba walipokwenda kwa ajili ya kufanya Utaratibu wa rufaa kwa Seneti kama walivyo elekezwa, seneti wamesema muda wa rufaa umeisha hivyo hawana muda wa kuendelea kupokea wala kusikiliza rufaa.

Aidha wanafunzi hawa wanalalamika kwamba kwa mfumo ulivyo hawakuwa namna ya kuingilia mfumo wa matokeo na kuubadili kama wanavgo singiziwa na uongozi wa CHUO

NI RAI YETU KWAMBA

1.Chuo Kikuu cha Dodoma ni Taasisi ya Umma ambayo inaongozwa kwa Mujibu wa Sheria na Kanuni ikiwamo maadili ya utumishi wa Umma na kwa msingi huo pia wanalazimika wakati wote kuzingatia matakwa na Masharti ya Sheria na Katiba ya Nchi.

2.Kwamba kwa hadhi ya Chuo hiki ni dhahiri kwamba wanatambua Msingi Mkuu wa Kikatiba kama unavyo onekana kwenye Ibara ya 9(a),(f) ,(h) ikisomwa pamoja na Ibara ya 13(6)(a) ya Katiba ya J̌amuhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu msingi wa kuzingatiwa wakati wa ufanyaji wà Maamuzi.

3.Kwambà haķi ya kusikilizwa ni pamoja na haki ya kujua kwa ufasaha tuhuma zinazokukabili mhusika na aina na asili ya tuhuma hizo ili aweze kuzijibu kwa ufanisi na kwamba Haki ya Kusikilizwa kwa haki inajumuisha haki ya kukata rufaa na kupewa uamuzi uliotolewa dhidi yako na sababu za uamuzi huo ili kukuwezesha kukata rufaa

4.Kwamba Seneti kukataa kupokea rufaa kwa sababu za jumla kwamba muda wa rufaa umekwisha bila kuzingatia muda ambao wa hanga hawa wamejulishwà kuhusu hatua na Maamuzi ya Chuo dhidi yao ni grave Injustice.

Tunatoa wito kwa Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dodoma kuchukua hatua za haraka kurekebisha na kulipatia ufumbuzi wa Haki tatizo hili ili kuzuia masuala ya Kitaaluma au shahada za Kitaaluma kwenda kutunukiwa Mahakamani.

CHUO CHA UMMA KINA WAJIBU MKUBWA ZAIDI WA KUULINDA UMMA na kuzingatia sana Maslahi mapana ya Umma na Misingi ya Haki wakati wote ili kujenga na kudumisha Maadili katika Utumishi wa Umma.

NI HATARI SANA KUPUUZA KADHIA YA WANAFUNZI 400.
Wanafunzi wengi ni makada wa vyama vya siasa! Hawasimi ,wanawaza siasa!


2. Walikotokea wamezoea mitihaninya multiple choice,wakifika huko wanakutana na nondo
 
Kwenye hili swala nasimama na UDOM wakizungua nasemaga na wakifanya vizuri napongeza ....kuna wanafunzi wahuni hawasomi hasa college za social na coed wakishikwa carry over mwaka wa mwisho au wakishindwa kuchomoa mitihani ya marudio yahn supplementary wanafanya uhuni huu na watu wa IT wa UDOM sio waaminifu (nahisi sina uhakika) wanafuta hizo sup na carry over kwa pesa.....kuna lectures wamekalili watuhumiwa wao akimuona mwakani hayupo lazima ujue hapa kuna michezo.

UDOM sio wajinga waanze tu kuwapiga hao wanafunzi DiSCO........

Rai kwenu viongozi wa chuo wakina prof Kusiluka mnajificha sana maofisini njoeni field kwa wanafunzi msikilize kero zao changamoto ni nyingi sana ŵatu wanakula mavyakula mabovu bei sio rafiki za wanafunzi na UDOSO(Serikali ya wanafunzi) ni machawa tu wa CCM hawajielewi wanaangalia etc.
Na kule social madukani bei wanabadili kila leo, sijui waliacha siku hizi mkuu?
 
Back
Top Bottom