Watu wana NOTION Mbaya sana juu ya OUT,Wanadhani kuwa wakikaa CUMPUS ndiyo kupata elimu bora.OUT siku hizi ni chuo cha kisasa sana,watu toka ujerumani,msumbiji,rwanda nk wako OUT.Sisi wenyewe wabongo tunaona kama ile ni TUITION centre hivi.Kiukweli ;
1.Out ni chuo kizuri na kimeboreshwa sana tofauti na miaka ya nyuma
2.Wahadhiri wake ni mahili sana
3.Kulingana na speed yako,unaweza kumaliza kozi kwa muda mfupi uwezavyo, mfano,nina ushahidi kuna mtu alimaliza masters kwa mwaka 1,na mwingine alimaliza postgr.Dip. kwa miezi 6.
4.OUTmwanafunzi anakuwa anauelewa mpana sana kwani hategemei VIDESA,anakamua vitabu zaidi tena vingi
5.Kwa watumishi walioko makazi na kusoma OUT wanapata promotion kirahisi kwa uzoefu wangu niliouna,
6.Out wana kozi nyingi na nzuri ambazo vyuo vilivyo vingi havitoi( cheki prospectus yao)
8.Gharama zao ni nafuu sana,
9.Unasoma huku unaendelea na madili yako
10.OUT ina scholarship za kwenda nje kwa masomo ya sayansi
11.Out ina maktaba,computer lab,kumbi za kusomea nk
12.Mimi ni miongoni mwa wanafunzi wa out(MASTERS),underg.nilisoma UDSM,HAKIKA, Naipenda Out.
13.OUT ni chuo cha serikali pia