Chuo kikuu cha Kampala tawi la Tanzania kimekuwa na tabia ya kuwatesa watanzania wanaosoma kozi mbalimbali hapo chuoni kwa kuwawekea mazingira magumu hasa inapofika nyakati za mitihani ili washindwe kufanya mitihani na badala yake wafanye mitihani ya marudio ambayo inalipiwa bei ghali sana.
Baadhi ya wanachuo wanaosoma ktk chuo hicho wameulalamikia utawala wa chuo hicho kwa kufanya matendo hayo ambayo yanawaumiza sana.
Mwanachuo mmoja ambae alionekana amechanganyikiwa alisema amezuiwa kufanya mtihani wa mwisho sababu tu eti anadaiwa hela za kulipia mtihani wa suppliment.
' Yaani nashangaa nimelipa ada yote ya chuo lakini naambiwa sitaweza kufanya mtihani wa mwisho kisa eti nadaiwa ada ya suppliment, kama nimeweza kulipa ada yote ya mamilioni nashindwaje kulipa ada ya suppliment kwa baadae?", aliuliza mwanachuo huyo. " "Kwa kawaida wanapaswa kuniruhusu nifanye mtihani wangu wa mwisho lakini wazuie cheti changu hadi hapo nitakapolipa hela hiyo ya suppliment "
Wanachuo hao wameuomba uongozi wa chuo kurekebisha hali hiyo na pia kuiomba mamlaka husika kutupia Jicho malalamiko hayo la watanzania wengi wataendelea kuumia.
PIA SOMA
- Kamwe USIJARIBU kusoma Chuo cha Kampala Dar es Salaam
- DOKEZO - Chuo Kikuu cha Kampala chini Tanzania kinawadhulumu wafanyakazi wake