Inasikitisha sana tunapoona viongozi waandamizi wa nchi hasa wabunge wakikubali kununua cheap doctorates kutoka vyuo vya kitapeli (rogue colleges). Hiyo inakupa picha kwamba hawa viongozi wetu hawajui hata kuangalia authenticity wakati kila kitu kipo online. Kwanza hiki sio chuo maana hakina address, hakina majengo na wala hakina makao makuu yanayoeleweka. Ni taasisi ya kijanjajanja tuu iliyoanzishwa na matapeli kwa ajili ya kuwatapeli watu wanaotaka umashuhuri nafuu hasa wa udaktari bila kutumia jasho
Hiki chuo kilichowapa udaktari wa heshima Mbunge Musukuma na wenzake kina kashfa ya siku nyingi ya kuuza hizi degree za heshima. Ukweli ni kwamba wanauza na sio wanatoa bure ama kulingana na mafanikio uliyonayo katika nyanja husika, wakati vyuo vyenye heshima zake na vinavyotambulika huwa vikitoa degree za heshima basi vinatoa na kiasi cha pesa ambayo kwa hapa Tanzania huwa ni pesa ndefu sana.
Hiki chuo kilichowapa udaktari wa heshima Mbunge Musukuma na wenzake kina kashfa ya siku nyingi ya kuuza hizi degree za heshima. Ukweli ni kwamba wanauza na sio wanatoa bure ama kulingana na mafanikio uliyonayo katika nyanja husika, wakati vyuo vyenye heshima zake na vinavyotambulika huwa vikitoa degree za heshima basi vinatoa na kiasi cha pesa ambayo kwa hapa Tanzania huwa ni pesa ndefu sana.
- Tunachokijua
- Udaktari wa Falsafa (PhD) duniani uko wa namna mbili. Mmoja ni kwa mtu mwenye shahada ya uzamili kujisajili katika Chuo ili kufanya tafiti ya kupata Shahada ya Uzamivu ambayo kwa jina lingine huitwa Udaktari wa Falsafa.
Namna nyingine ni mtu kutambuliwa kwa mchango wako katika jamii au suala fulani, udaktari huu wa falsafa huitwa Udaktari wa Heshima 'honoris causa' ambao hauhusiani na taaluma. Baadhi ya watu wenye udaktari wa heshima ni pamoja na Marehemu Dr. Reginald Mengi (Tanzania), Dr. Oliver Mutukudzi (Zimbabwe), Dr. Jose Chameleone (Mganda).
Japo PhD ya heshima haina uhusiano na taaluma, hutolewa na taasisi za juu kitaaluma (Vyuo Vikuu). Awali, mtu aliyekuwa anapewa Udaktari wa heshima hakuwa anatumia neno Daktari, lakini utaratibu wa hivi karibuni watu wengi wamekuwa wakitumia Dokta kabla ya majina yao. Na likawa suala ambalo watu wengi kutoka Afrika wanalipenda kuwa na jina Daktari kabla ya jina lake.
Mbunge wa Geita Vijijini, Joseh Musukuma alitunukiwa Udaktari wa Heshima na Chuo cha Marekani (American college, ambacho pia kinajulikana kama Academy of Universal Global Peace). Taarifa hizi zilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii Disemba 5, 2021 ambapo mdau wa JamiiForums aliweka pia chapisho lenye kichwa cha habari "Mbunge wa Geita Vijijini atunukiwa Udaktari wa heshima, sasa kuitwa Dkt. Joseph Kasheku"
Akizungumza baada ya kupokea heshima hii, Musukuma alisema;
“Mimi nimepata PhD yangu ya Siasa na Uongozi. Na mimi ni Mbunge ambaye kwenye Bunge letu nimekuwa nikiwa-challenge sana Madaktari na Maprofesa. Sasa kwa vile nimekuwa na mimi Dokta ninaamini na mimi siku moja watakubali nitoe mhadhara ili waweze kusikiliza ninayoyasema kwa sababu ni Daktari mwenzao.
Lakini hili pia ni fundisho kwa vyuo vyetu vya Tanzania. Tanzania tunavyo vyuo vingi sana. Leo tunasheherekea miaka 60 ya uhuru, tujiulize Maprofessa na Madaktari wa vyuo vikuu ni Watanzania wangapi wenye uwezo kama Musukuma – wa kujenga hoja, wa kusaidia watu, ambao mmeweza kuwatunuku tuzo kama hii? Jibu linakuja mna wivu na watu wanaofanya kazi vizuri. Naona hata waandishi wengine wananionea wivu.”
Baada ya kusikika kwa habari hii, mjadala mkubwa umeibuka kwenye mitandao ya kijamii ukihoji uhalali wa chuo hicho, na kama Musukuma alistahili kupewa heshima hiyo.
Historia ya chuo hiki katika kutoa udaktari wa heshima ipoje?
Chuo hiki kwa nyakati kadhaa kimekumbana na tuhuma za uuzaji wa udaktari Udaktari wa heshima kwa viongozi wengi duniani, hasa wale wanaotoka bara la Afrika.
Mathalani, July 28, 2018, Gazeti la Chub Magazine lilichapusha makala inayotia shaka uthabiti wa udaktari wa heshima waliokuwa wanapewa wanasiasa na Watu Mashuhuri nchini Nigeria.
"Baadhi ya Wanigeria mashuhuri huko London, ambao wengi wao ni viongozi wa jamii, wanasheria na waigizaji wa Nollywood wamenaswa katika udaktari bandia wa heshima kwani uhalisi wa taasisi hiyo na tuzo zake zimetiliwa shaka.
Heshima hiyo iliyofahamika kwenye jamii mwaka jana imeuza zaidi ya tuzo 20 kwa Wanigeria wengi kati ya mwaka wao wa mwisho na sherehe ya mwaka huu. Wasomi wanaojali walitilia wasiwasi tuzo hizo wakati picha zilipoibuka za wapokeaji wa tuzo ya heshima ya mwaka huu zilikuwa na umuhimu wa kutiliwa shaka. Wakati hadithi hiyo ikiendelea kuibuka, inakadiriwa kwamba waliopokea zawadi walikuwa wamelipa kila mmoja, kiasi cha pauni 2500 (karibu shilingi milioni 8 za kitanzania) kupokea heshima hiyo."
Chuo hicho, Academy of Universal Global Peace ambacho kinadai kuidhinishwa na serikali ya Uingereza, Marekani, na India pamoja na Umoja wa Mataifa kinasemekana kuanzishwa na 'Mtukufu' wake Dk. Madhu Krishan mwaka wa 1985, ambaye inadaiwa kuwa pia ni Rais wa Asia 'Power Ministries Intl, Inc. Marekani na anashikilia nyadhifa kadhaa katika mashirika mengi ya kimataifa, baina ya serikali. Dai la heshima kwa jina la mwanzilishi linaendelea na kuendelea, hata hivyo, swali ambalo bado halijajibiwa ni je, ni chuo kikuu gani kimeidhinisha taasisi hii kutoa udaktari wa heshima?
Juhudi za JamiiForums katika kulijibu swali hili zimegonga mwamba kutokana na kukosekana kwa uthibitisho wake.
Aidha, Chuo Kikuu kilichopo Japan kinachoitwa United Nations University kiliwahi kukanusha pia madai ya AUGP baada ya kuadai wana ubia kati yao. Huu ni uthibitisho mwingine unaoonesha kuwa chuo hiki sio cha kuaminika.
Haijulikani makao yake makuu ya chuo hiki yapo wapi. Je, ni Marekani au India?
Kanusho la United Nations University kujihusisha na American University for Global Peace
Sehemu fulani wanaonesha kuwa makao yao makuu yapo New Jersey nchini Marekani lakini kwingine wanasema kiongozi wao mkuu huwa anahamahama na kwa sasa yupo India. Kwa hiyo, makao makuu ya chuo yapo Chennai. Vile vile, chuo kinaonekana kuwa na tovuti zaidi ya moja, hivyo kufanya upatikanaji wa taarifa za uhakika kuwa mgumu.
Suala hili liliibuka hadi Bungeni Februari 9, 2023 ambapo Spika Tulia alisema ifike mahali wao kama viongozi wawe na haya, wajue jamii inawangalia kama kioo masuala ya kununua vyeti waachane nayo.
“Kama taifa ifike mahali tujue tunataka nini? Athari zake tunaweza tusizione sasa tukaziona kesho, UDSM inapompa Rais degree ya falsafa ya heshima ujue kuna proposal imeandikwa, jopo linakaa linafanya tafiti ya kazi alizofanya tangu alipoanza kufanya kazi mpaka alipofika, wanapima kwa vigezo vyao kama anafaa kupewa au la.
Iitafika mahali wanaolipa pesa Dola 2500 hawatakua na tofauti na anayopewa Rais. Halafu mna watoto, mmewapeleka shule ili wasome waelimike tena mnawakazania kusoma kwa bidii, huku nyie mnanunua vyeti, mnapeleka watoto shule kufanya nini? mnawafundisha nini watoto wenu? Kwamba elimu haina maana watafute pesa wanunue cheti.
Waheshimiwa Wabunge, vyuo vinavyotambulika havitoi degree kila wiki kila mwezi, uliza UDSM au UDOM toka wameanza wametoa degree za falsafa mara ngapi?"
Spika Tulia alibainisha kuwa sio tu vyuo vya nje wanakuja na makabrasha yao ya vyeti wanaviuza kama pipi, kana kwamba vyuo vyetu havina umuhimu, kama taifa tuweke mwongozo mzuri, Tanzania sio kijiji vinakotoka hivyo vyeti wangeanza kutoa huko nchini kwao, wageni kuja na kuuza vyeti vyao kama pipi hapa ni kutuvunjia heshima kama nchi.
Aidha, alisema hazuii wanaotaka kuendelea kununua vyeti hivyo.
Pamoja na Musukuma, Wabunge wengine waliowahi kutunukiwa shahada ya heshima ni pamoja na mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki, Hamis Taletale maarufu kama Babu Tale, mbunge wa Morogoro Mjini, Abdulaziz Abood na mbunge wa viti maalumu (CCM), Ritha Kabati ambaye alitunukiwa katika Bunge lililopita