- -ve yangu kubwa sipendi kusimamiwa ninapopewa/ninapofanya kazi fulani iwe oficini au nyumbani,huwa ninaamini kama ni kitu kipya ukishanipa directives,siwezi kushindwa(niache uone kama nitashindwa,na nikishindwa si nitauliza?),sio unakaa nyuma ya mgongo wangu,unaamrisha"do this",no......no this way, mara that way,aaaugh.Yaani naweza kuacha kila kitu.Nikakutizama tu tena kwa hasira(sijui kwanini huwa naamini naweza, na ni mtu wa kujituma hasa)
- Ya pili,hata kama nimekosea,sipendi ushout huku ukiwaalert wengine how bad it was.If you do this "sitaapologize",and i will hate you.(Nieleze kosa kwa upole tena tukiwa mi and yu,hapo nitaomba msamaha mara mia).Hii husababisha wengine waone sipendi kuambiwa ukweli,kumbe ni approach waliyotumia imesababisha hivyo.
3. Nikiamini jambo fulani kuwa liko hivi,na ninalielewa vizuri na ushahidi ninao,hata ubishane nami jan-dec,sibadiliki.Zaidi sana nitaendelea kutafuta more evidence nikubadili wewe.
4. Mwepesi mno wa kusamehe,niko very understanding cha msingi muhusika awe mkweli,akiri na kuonyesha nia ya kubadlikika(hata kama nimeolewa then mume akaleta mtoto wa nje aliyezaliwa tukiwa ndoani),nitamsamehe.Nashindwa kuhukumu.
naona kama niko weak sana hapa,yaani moyo wangu ndivyo ulivyo mwenzenu sijui nifanyeje.
5. Mtu akiniudhi,awe ndugu,jamaa n.k (japo kuniudhi ufanye kazi haswaaa),nitakasirika,naweza kuwa na majibu ya mkato kwake ili nisitamke neno baya kutokana na hasira,huku najiuliza
moyoni,"hivi hajui kama kaniudhi?",then baada ya muda,masaa n.k nikiona haelewi "nasamehe hukohuko moyoni",alafu naendelea na maongezi naye kama kawaida then ndio nitaweza mwambia kama aliniudhi na nimeshasamehe lakini hapo kumbuka
nilishaumia ile mbaya "kimoyomoyo"
Nifanyeje niweze kubadilika,au nifanyavyo ni sahihi