Huku uswahilini tunakoishi haiwezekani maana choo/bafu ni vya kugombania.mnaanikaje chupi nje jamani...chupi,soksi pamoja na taulo vinaanikwa bafuni tena unafunga taa maalum kwa ajili ya kukausha na kuua bacteria
sio theoretical ndugu ulimwengu mkubwa zunguka uone teknolojia...ushawahi jiuliza zile nchi za baridi kali inayoambatana na snow huwa wanakausha vipi nguo
Sehemu bora ni nje juani ili ikauke vizuri......!
Upige na pasi.......!!
Salaam wa JF,
binafsi napenda na sipendi mtu asiye wangu aione chupi yangu pasipo sababu ya msingi, lkn nakuta jirani yangu yeye anafua na hupenda kuanika chupi zao (mke na mume ) nje ktk kamba, siku moja nikamuuliza kwa nini anaanika nguo ya ndani nje haoni kuwa anajivunjia heshima kwa watu na watoto, sikumuona kujali, nawauliza wenzangu ni ipi sehemu bora ya kuanika chupi............!!
Duh, sikuwezi mwali wewe! Utatufunda siku tunakuoza. Sijawahi kupiga pasi pichu in my life! Sasa zile za nanihii si unam
Panga 10 afu unalalisha pasi? Hongera mamito!
Kwny kamba ili ipate hewa na kuua vijidudu, ikikauka nenda kainyooshe
sianiki kwa sababu natumia dispozabo.....
Naanika nje kwenye kamba baada ya kuifua jioni na kuikamua sawa sawa ili kesho niivae tena.
Mi ninazo kama thelathini hivi, navaa zikifika 15 zimechafuka nafua na kuanika hizo 15 zote nje kwenye kamba,then zikifika 15 tena kama kawa,kama una muda wa kuzishangaa nikianika kwenye kamba sawa we endelea ila ziko 30,hauwezi kuzijua zote na hata ukiziona kwenye kamba kesho nikitoka hauwezi kujua nimevaa ipi, ni mke wangu tu anayeweza kujua hivyo unabaki kuwa kama haujaona tu!
mh.......sasa huku kwangu kwa bi nyau, nikianika kapichu kangu haka ka vikamba kamba tu cjui ndio mnaitaje NAAMBIWA nawatega waume wa wenzangu..................
ukisema sayansi kimu kizaz cha leo ni MSAMIAT MPYA HUO,,,,,ILA ILE ILIKUA NI ELIMU BORA SANA,HADI SASA NAKUMBUKA HATUA ZA KUFUA NGUO MFANO SHATI AU SURUALI,UNAANZIA WAPI HADI WAPI