Chura kiziwi naye hutuoa sauti kama chura wengine tu

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
21,470
Reaction score
40,593
Kwenye siasa wanasiasa huibua misemo ambayo mingine huja kuwa sehemu ya Lugha husika.

Mchungaji Christopher Mtikila alileta misemo ya "Gabacholi" na "mlalahoi" na la mlalahoi linatumika mpaka Sasa.

Mwalimu Julius Nyerere alileta kwenye lugha ya kiswahili msemo wa "kung'atuka" na "tapeli" na yote miwili imekuwa sehemu ya misamiati ya lugha ya Kiswahili.

Sasa kumekuja msemo mpya wa "chura kiziwi" kutoka kwenye hotuba ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Kiuandishi na kiuchanganuzi kifasihi, chura kiziwi ni Hali/tabia ya mtu kutokujali makelele ya watu wengine kwenye kile akifanyacho na anachoamini kuwa kiko sawa.

Kifasihi vile vile, chura huishi zaidi kwenye madimbwi na vyura wengine. Kwa ivo kuwa chura kiziwi hakuondoi tabia nyingine za Shani za kimaumbile za chura.

Kwa ivo ingawa chura kiziwi hasikii makelele ya vyura wengine, lakini kimsingi ule uchura wake humfanya naye atoe sauti ya makelele ya kukoroma kama vyura wengine.

Kikawaida binadamu na wanyama wengine wasio viziwi, wapitapo kando ya dimbwi watasikia makelele ya vyura bila ya kujua kuwa kumbe mmoja wa vyura hao ni kiziwi.

Ni mambo ya fashihi ya kisiasa.

=====

Pia soma:

- Rais Samia: Wananitukana ili niwajibu, najigeuza chura siwajibu
 
20240820_145755.jpg
 
Back
Top Bottom