Chura wa Kihansi na safari ya Marekani

Chura wa Kihansi na safari ya Marekani

Ryan Holiday

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2018
Posts
2,026
Reaction score
4,450
CHURA WA KIHANSI
  • Taxonomy
👉Kingdom⟹ Animalia
👉Phylum ⟹ Chordata
👉Class ⟹ Amphibia
👉Order ⟹ Anura
👉Family ⟹ Bufonidae

Vyura wa kihansi kwa jina la kisayansi wanajulikana kama "Nectophrynoides asperginis" ni aina ya vyura wadogo ambao wanapitikana Tanzania tu, katika mkoa wa Iringa kwenye bonde la mto Kihansi na chakula chao ni wadudu (insectivorus). Chura wa kihansi ni chura pekee katika jamii ya vyura waliopo duniani kwa sababu vyura hawa hutaga mayai na kukaa nayo kwenye kifuko kilichopo ndani ya chura mwenyewe hadi muda wa kuanguliwa unapofika na ndipo hutoa vitoto hai.Kwa lugha rahisi ni kwamba Chura hawa huzaa kwa sababu hatagi mayai yakaonekana bali hukaa ndani ya chura mwenyewe.

IUCN (International Union For Conservation of Nature) walifanya utafiti na kugundua kuwa vyura wa kihansi wapo kwenye hatari kubwa ya kutoweka (Extinct in the wild). Awali uharibifu wa makazi yao ya asili uliotokana na utengenezaji wa bwawa la Kihansi kwa ajili ya kuzalisha umeme ulionza mwaka 1995 na kukamilika mwaka 2000 na kupelekea kupungua kwa kiasi kikubwa cha maji kwa asilimia 90 ambacho kilikua kinatiririka kutoka kwenye maporomoka ya bonde la mto kihansi. Lakini taarifa nyingine za waatalamu zinataja kuwa sababu za kutoweka kwao huenda zilisababishwa na utumiaji wa mbolea za kikemikali (artificial fertilizer) katika vyanzo vya maji yanayotiririka katika mto huo. Huku pia huwepo wa aina fulani ya fungus wanaojulikana kama chytrid. Hata hivyo mradi huo wa umeme ulisababisha uharibufu wa makazi yao ya asili na kusababisha kukosekana kwa unyevu nyevu wa kutosha na kupungua kwa mimea katika bonde hilo.

Matokeo ya uchunguzi wa IUCN kwa kutumia miongozo ya "IUCN RED LIST CATEGORIES AND CRITERIA":-
2004→ Critically Endangered (CR)
2006→ Critically Endangered (CR)
2009→ Extinct in the wild (EW)

Vyura wa kihansi kutokana na uharibifu wa makazi yao ya asili. Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na wadau wengine wa mazingira kama vile World Conservation Society na Benki kuu ya Dunia walianzisha project ambapo takribani vyura 500 walichukuliwa na kupelekwa Marekani kwa ajili ya kuhifadhiwa na kuongeza idadi yao hili kuzuia athari ya kutoweka duniani, waligawanywa na kuhifadhiwa katika Zoo sita huko Marekani. Bronx Zoo na Toledo Zoo ndizo ambazo ziliweza kuwahifadhi na kufanikiwa kuongeza idadi yao. Maonyesho ya kwanza ya Vyura wa Kihansi nchini Marekani yalifanyika katika Toledo zoo mwaka 2005. August mwaka 2010 kundi kubwa la vyura wa kihansi walisafirishwa kutoka Bronx Zoo na Toledo Zoo mpaka Tanzania na kuhifadhiwa katika chuo kikuu cha Dar-es-salaam kwa ajili ya uzalishaji na kuongeza idadi yao kabla ya kurudishwa katika makazi yao ya asili.

1. Je, wewe kama mdau wa mazingira na maliasili za nchi ya yako, je kulikuwa kuna ulazima wa vyura hawa kusafirishwa na kupelekwa nchini Marekani na wakati Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam kulikuwa na maabara ambayo ingeweza kuongeza idadi yao kama walivyofanikiwa kuongeza idadi hiyo na kuwarudisha katika makazi yao ya asili?
2. Na bado tunaendelea kusema ni vyura pekee wanaopatikana Tanzania tu, kama nilivyotype mwanzoni mwa uzi huu. Kama waligawanywa katika Zoo 6 nchini Marekani na Zoo 2 tu kati ya hizo 6 ndizo zilifanikiwa kuongeza idadi yao. Kwa nini hizo zoo 4 zilizobaki walishindwa kuongeza idadi yao maradufu?
3. Je, wasomi wetu wa wildlife management wa SUA, MWEKA na UDSM walishindwa wapi kuhusiana na uhifadhi na uzalishaji wa vyura hawa na kupelekea kusafirishwa mpaka nchini Marekani?
4. Je, kama ni issue ya teknolojia na vifaa vya uhifadhi na uzalishaji wa vyura hao, walishindwa kuviinstall hapa hapa katika maabara zetu na kupunguza usumbufu na gharama za usafirishaji wa vyura hao?

Namalizia kwa kusema kwamba Wazungu sio wajinga hata kidogo.
 
Maswali uliyouliza ni ya msingi tusubiri majibu lakini pia tujiulize ni nani aliegundua kwamba wapo hatarini kupungua?kama ni wazungu na sio wataalamu wetu uliowataja hapo juu basi vyura walistahili kusafirishwa maana kazi ilishawashinda

Na kama ni wataalam wenyeji ndio waligundua walishindwa vipi kuzalisha hapahapa kama maabara ipo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bado nafikiria sisi kama Taifa tunakwama wapi?
 
Nilisikiaga hao vyura wakihamishwa eneo lao wanaloishi wanaacha kuzaa wanakua wanataga mayai kama vyura wengine.
Sijui zilikua story za vijiweni pale bomaroad
 
Mkuu, nilipo soma "chura" mawazo yangu yaliwaza mbali sana... basi Mungu anisamehe tu, maana sio kwa baridi hili[emoji4][emoji4]
Chura......? Na hapa kwenye Safari ya Marekani uliwaza nini?
 
Nilisikiaga hao vyura wakihamishwa eneo lao wanaloishi wanaacha kuzaa wanakua wanataga mayai kama vyura wengine.
Sijui zilikua story za vijiweni pale bomaroad
Chura wa kihansi ni chura pekee katika jamii ya vyura waliopo duniani kwa sababu vyura hawa hutaga mayai na kukaa nayo kwenye kifuko kilichopo ndani ya chura mwenyewe hadi muda wa kuanguliwa unapofika na ndipo hutoa vitoto hai.Kwa lugha rahisi ni kwamba Chura hawa huzaa kwa sababu hatagi mayai yakaonekana bali hukaa ndani ya chura mwenyewe.
 
Nawafahamu vizuri tu. Sema kama vile hujaelewa nilichosema.
Mimi nilisikia hawa vyura wakitolewa hapo kihansi hua wanakua kama vyura wengine kwenye upande wa uzalishaji. Ndio nikauliza kama story ya kweli au porojo za vijiweni.
 
Porojo za vijiweni mkuu, huo ndio mfumo wao wa Reproduction, fertilization lazima itokee internal na ukuaji wa tadpoles ufanyika ndani pia mpaka pale watakapo kuwa chura kamili (small toad's) ndio utolewa nje ya mfumo wa uzazi (uzaliwa).
 
Basi tukawa tunaona ni miujiza kweli [emoji28][emoji28]
 
John Joba kwa kipindi kile walipohamishiwa USA, hapa Tz wataalamu wetu hawakuwa na capacity ya kuwalea na kuwakuza hao vyura.

Ukumbuke walitoka 'porini' na hakuna aliyekuwa anajua aina ya vyakula au mahitaji yao yalikuwa kivipi. Hata hao wa Toledo na Bronx walifanya kazi kubwa sana na utafiti kuweza kudocument taarifa zao, na kuna kipindi walibakia 72 tu katika captive facility yao. Tim Hermann aliandika papers kuhusu utunzaji wa vyura hawa.

Hata hivyo NEMC kwa kushirikiana na UDSM na SUA walijenga uwezo wa wataalamu wa nchi hii kuweza kuwatunza, kuwaendeleza na kuwarudisha porini kwenye makazi yao ya asili.
 
Kumbe hii issue ya vyura ndio ilipelekea yule baba kulalamika kila mara kuwa
'Tumeibiwa sana ndugu yangu'
 
Back
Top Bottom