Kilembwe
JF-Expert Member
- Aug 19, 2009
- 2,058
- 1,609
Nashukuru kwa ufafanuzi..kwa kuongeza tu ni kuwa wakati wale vyura wako Marekani tafii ziliendelea kwa kiasi kikubwa sana huku Tanzania juu ya chanzo hasa cha kupungua kwao kule porini. Hawa chura kule kiasi walikuwa wanapatikana katika bonde moja tu na moja ya mahitaji yao ya mazingira ni "wetness ya eneo lao", watu wa lower Kihansi wakaweka spray ili kuwawekea huo unyevu lakini bado walitoweka, na baadae ikagundulika pia wanashambuliwa sana na fungus, na ikabidi liwekwe sharti la "kuosha" viatu kwa kukanyaga dawa ukiwa unapanda kule mlimani. Badaa ya hapo UDSM walipeleka Mtaalam pale Brox Zoo na baada ya ghrama za kuwatunza kuwa kubwa na kuonesha uwezo wa kuzaa vizuri wakiwa in captivity ndio, serikali ya Tanzania kwa ushirikiano na World bank wanakubaliana kujenga maabara ya kuwatunza pale UDSM na kule Kihansi. Ila kwa sasa idadi kubwa iko Kihansi chini ya uangalizi wa Tawiri.John Joba kwa kipindi kile walipohamishiwa USA, hapa Tz wataalamu wetu hawakuwa na capacity ya kuwalea na kuwakuza hao vyura.
Ukumbuke walitoka 'porini' na hakuna aliyekuwa anajua aina ya vyakula au mahitaji yao yalikuwa kivipi. Hata hao wa Toledo na Bronx walifanya kazi kubwa sana na utafiti kuweza kudocument taarifa zao, na kuna kipindi walibakia 72 tu katika captive facility yao. Tim Hermann aliandika papers kuhusu utunzaji wa vyura hawa.
Hata hivyo NEMC kwa kushirikiana na UDSM na SUA walijenga uwezo wa wataalamu wa nchi hii kuweza kuwatunza, kuwaendeleza na kuwarudisha porini kwenye makazi yao ya asili.
