Chura wa Kihansi na safari ya Marekani

Nashukuru kwa ufafanuzi..kwa kuongeza tu ni kuwa wakati wale vyura wako Marekani tafii ziliendelea kwa kiasi kikubwa sana huku Tanzania juu ya chanzo hasa cha kupungua kwao kule porini. Hawa chura kule kiasi walikuwa wanapatikana katika bonde moja tu na moja ya mahitaji yao ya mazingira ni "wetness ya eneo lao", watu wa lower Kihansi wakaweka spray ili kuwawekea huo unyevu lakini bado walitoweka, na baadae ikagundulika pia wanashambuliwa sana na fungus, na ikabidi liwekwe sharti la "kuosha" viatu kwa kukanyaga dawa ukiwa unapanda kule mlimani. Badaa ya hapo UDSM walipeleka Mtaalam pale Brox Zoo na baada ya ghrama za kuwatunza kuwa kubwa na kuonesha uwezo wa kuzaa vizuri wakiwa in captivity ndio, serikali ya Tanzania kwa ushirikiano na World bank wanakubaliana kujenga maabara ya kuwatunza pale UDSM na kule Kihansi. Ila kwa sasa idadi kubwa iko Kihansi chini ya uangalizi wa Tawiri.
 
Kitu nilichojifunza kwa Wazungu (White people) jambo linaweza likawa simple and clear, lakini wao wakalifanya lionekane ni jambo gumu sana kutekelezeka with alot of complications.
Lengo kuu ni hili ukubali mawazo yao na ideology yao kwenye jambo lao na hatimaye kufanikisha mipango yao juu ya jambo lao.

Nipende kunukuu kidogo moja kati ya sentesi yako bitimkongwe ''Ukumbuke walitoka 'porini' na hakuna aliyekuwa anajua aina ya vyakula au mahitaji yao yalikuwa kivipi''.

Je, walishindwa kujua aina ya chakula chao na mahitaji yao?

Tuna wataalam wengi tu wenye Intellectual ability ya Wildlife Conservation, Environment Science pamoja na Forest Conservation.
Kama wanyama kama Simba, Chui, Duma, Paka mwitu na Fisi (ni wanyama walao nyama - Carnivorus) na ukitaka kujua mahitaji yao lazima ufanye utafiti katika ecosystem yao.
Most of Class Amphibians (Vyura) ni wanyama walao wadudu - (Insectivorus) na ukitaka kujua mahitaji yao lazima ujue ecosystem yao - Interaction between biotic and abiotic components around they are surrounding.

Nafikiri changamoto kubwa kwetu ingekuwa Technological Factor (Well Equiped Instruments for Restoration) lakini nyingine ni possible zinawezekana.

So nafikiri kila jambo ni uthubutu tu ukiamini unaliweza na itakuwa hivyo, ukiamini you are not well prepared to tackle that kind of challenge na itakuwa hivyo hivyo pia.

That's why ''Fortune favours the Brave''
 
Most of Class Amphibians (Vyura) ni wanyama walao wadudu - (Insectivorus) na ukitaka kujua mahitaji yao lazima ujue ecosystem yao - Interaction between biotic and abiotic components around they are surrounding
Easier said than done. Na wala siyo kuwa nadharau utaalamu wa wanasayansi wetu, lakini vitu kama mahitaji yao maalumu kwenye ecoystem yao (mfano, ule unyevu) vilikuwa havikueleweka hapo awali. Hata hizo fedha za kugharamia huo utafiti wa awali zisingetolewa na serikali kwa ajili ya chura. Ungeambiwa hiyo siyo kipaumbele.
 
Tumeaminishwa hivyo na itaendelea kuwa hivyo?

Tatizo kidogo tunaomba misaada kwa wenzetu ambao na wao pia wanachangamoto zao kwa sababu nobody is free from problem.

Hakuna cha bure in this world of Capitalism, chochote wanachokifanya kwa ajili yetu sio kwa ajili yetu bali ni kwa ajili yao. Kwa sababu super power anataka aendelee kuwa super power na sisi Kama Third world Country we must pay that price.
 
Bitimkongwe kwa sasa serikali inagharamia hawa chura kwa kiasi kikubwa sana, wanatumia umeme 24/7, kuna siku umeme ulikatika katika maabara yao pale Kihansi kwa sababu jenerata wanalotumia lilileta shida, ilibidi jenereta ya dharura ikimbizwe kule kutoka Morogoro mjini...kwa agizo la serikali!
 
Utakuta Sasa Marekani ndo itakuwa inaongiza kwa kuwa nao wengi
 
Sasa huko Marekani hawapo maana nao waliwaona Tanzania kwa mara ya kwanza,huo utaalami wa kutunza waliupata wapi? Hapa ni uhakika kwamba tulipigwa.
 
Sasa huko Marekani hawapo maana nao waliwaona Tanzania kwa mara ya kwanza,huo utaalami wa kutunza waliupata wapi? Hapa ni uhakika kwamba tulipigwa.
Haikuwa rahisi....waliwatengenezea artificial environment maabara na ilikuwa kama trial and error, walikufa sana kipindi cha mwanzo na ilichukua muda hadi walipoanza kuzaliana huko maabara
 
KIHANSI FROG ARTICLE

The Dynamics of Re-introduced Kihansi Spray Toad Nectophrynoides asperginis and other Amphibians in Kihansi Gorge, Udzungwa Mountains, Tanzania

Wilirk Ngalason, Cuthbert L Nahonyo and Charles A Msuya.
Department of Zoology and Wildlife Conservation
,
University of Dar es Salaam,
P. O. Box 35064, Dar es Salaam,
Tanzania.
Corresponding author, e-mail: wilirk@udsm.ac.tz
 

Attachments

Nilisikiaga hao vyura wakihamishwa eneo lao wanaloishi wanaacha kuzaa wanakua wanataga mayai kama vyura wengine.
Sijui zilikua story za vijiweni pale bomaroad
Ulidanganywa
 
Haikuwa rahisi....waliwatengenezea artificial environment maabara na ilikuwa kama trial and error, walikufa sana kipindi cha mwanzo na ilichukua muda hadi walipoanza kuzaliana huko maabara
Kweli kabisa na hapa issue ilikuwa ni financial muscle. Je Serikali ya Tz ingeweza kutoa fedha nyingi zile kwa kufanyia majaribio tu ya ecolojia ya chura? Utafiti ulichukua kama miaka tisa kabla ya kupata population ya kutosha kuweza kuwarudisha Tz, je hizo fedha zingetolewa na serikali yetu?

Unaweza kuuliza ni faida gani kwao wanapata? Kwanza kwa kuwa wao ni wataalamu wenye uzoefu wa muda mrefu kwa hivyo wanajiongezea umaarufu. Pili wao wakiomba fedha kwenye serikali yao kwa ajili ya utafiti ni rahisi kupatiwa. Tatu wale vyura wako kwenye zoos (Toledo na Bronx) ambazo zinaingiza fedha kwa mamilioni na hao vyura ni sehemu ya vivutio katika hizo zoos.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…