CIF, Cost, Insurance, and Freight Ghalama za kutoa gari kiwandani mpaka bandari A, upakiaji, usafirishaji mpaka ushushaji kwenye bandari B zinalipwa na muuzaji. Wewe utafidia ghalama hizo unapomalizia malipo ukipata mzigo, vile vile uharibifu au upotevu wa mzigo utakua ni juu yao.
FOB Free on board Kampuni itapokea malipo na wewe mnunuzi utatakiwa utafute wakala wa usafirishaji ambae atashughulikia kila kitu mpaka unapata mzigo, vile vile kampuni haitahusika kwa namna yoyote iwapo mzigo utaharibika au kupotea.
Kuhusu miamala ya kibenki huwa wanatoa namna ya kufanya malipo ila inashauriwa utumie wataalamu wa huduma hizo. Hii ni kitokana na biashara ya matandao kuwa na changamoto nyingi.