CIIE kuunga mkono Afrika kuungana zaidi na uchumi wa dunia

CIIE kuunga mkono Afrika kuungana zaidi na uchumi wa dunia

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
VCG111522916506.jpg


Katika mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) uliofanyika Beijing mwezi Septemba mwaka huu, China ilitangaza mpango wa kufungua zaidi soko lake na kuzipa msamaha wa ushuru wa forodha bidhaa zinazoagizwa kutoka nchi zilizo nyuma kimaendeleo, zikiwemo nchi 33 za Afrika. Uuzaji nje wa bidhaa za kilimo ni njia muhimu kwa nchi za Afrika kuungana na uchumi wa dunia. Kama jukwaa muhimu la China kufungua mlango wake kwa nje, Maonyesho ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China CIIE yanayotarajiwa kufanyika Shanghai kwa awamu ya saba yatasaidia bidhaa za kilimo za Afrika kuingia kwenye soko la China kwa njia rahisi zaidi.



Katika mazingira ya kimataifa ya sasa, maendeleo ni suala muhimu sana kwa nchi nyingi duniani, hasa kwa nchi za Afrika. Kwa mujibu wa waandaaji, maonyesho ya CIIE kwa mwaka huu yatapanua zaidi eneo la bidhaa za Afrika, ili kusaidia wafanyabiashara wa Kiafrika kuingia mikataba zaidi na wanunuzi wa Kichina na kuanzisha ushirikiano wa muda mrefu. Ni vyema kutaja kwamba baada ya maparachichi ya Kenya na Tanzania kuonyeshwa katika awamu mbili zilizopita za Maonyesho hayo na kufanikiwa kuingia kwenye soko la China, mwaka huu kilo 22,000 za maparachichi safi kutoka Afrika Kusini pia zimeifika Shanghai kama kituo cha kwanza kuingia soko la China na zitaonekana kwenye maonyesho ya CIIE.



“safari ya maparachichi ya Kiafrika” kwenye Maonyesho ya CIIE ni mfano wa jinsi China na Afrika zinavyoshirikiana kuchangia fursa ya soko la China. Tangu mwaka huu kuanza, China imesaini makubaliano ya uagizaji wa bidhaa za kilimo na nchi 14 za Afrika, na kati ya Januari na Agosti, uagizaji wa China wa bidhaa za kilimo kutoka Afrika ulifikia dola za kimarekani bilioni 4, ikiwa ni ongezeko la asilimia 4.8 kuliko mwaka uliopita kipindi kama hicho. Katika mkutano wa 16 wa viongozi wa nchi za BRICS uliomalizika hivi karibuni, Rais Xi Jinping wa China alisisitiza tena msimamo wa China wa kuweka maendeleo katika msingi wa ajenda ya biashara ya kimataifa, jambo ambalo linaendana na juhudi za China za kusaidia Afrika kuinua nafasi yake katika minyororo ya thamani duniani.



Lakini kinyume na msimamo wa China, Marekani na nchi nyingine za Magharibi zimechukua hatua mbalimbali za kujilinda kibiashara, jambo linaloweza kurudisha nyuma uchumi wa dunia. Hii inazifanya nchi za Afrika, hasa zile zilizo na uchumi mdogo, kukumbwa na changamoto kubwa ya kuingia kwenye masoko ya kimataifa. Katika muktadha huu, China imeanzisha maonyesho ya kwanza ya kitaifa yenye lengo la kuagiza bidhaa kutoka nje yaani CIIE na tangu awamu ya kwanza imealika nchi mbalimbali kushiriki, ikitoa hatua mbalimbali bora kama vile mabanda ya bure na punguzo la ushuru ili kusaidia bidhaa za nchi hizo kuingia kwenye soko la China. Mbinu hii inadhihirisha kikamilifu dhana ya msingi ya sera ya ushirikiano wa kimataifa ya China yaani uwazi, ujumuishi, na ushirikiano wa kunufaishana.



Hali halisi ni kuwa si CIIE tu, bali pia majukwaa kama vile Maonesho ya Uchumi na Biashara ya China na Afrika na Tamasha la Bidhaa Bora la Afrika yaliyofanyika miaka ya hivi karibuni ni madirisha ambayo China inaandaa kama fursa kwa bidhaa za Afrika kujitangaza. Wachina husema "kwa sababu niliwahi kunyeshewa na mvua, hivyo niko tayari kuwashikilia mwavuli wengine." China imeendelea kutoka nchi maskini ya kilimo hadi nchi ya pili kiuchumi duniani, na inafahamu zaidi umuhimu wa uchumi wa dunia ulio wazi kwa maendeleo ya nchi. Inaaminika kuwa kadiri soko la China linavyoendelea kufunguliwa nje kwa kiwango cha juu, bidhaa zaidi za nchi za Afrika zinazojenga BRI kwa pamoja zitaingia kwenye soko la China kupitia majukwaa haya, na kupata umaarufu mkubwa miongoni mwa watu wa China.
 
Back
Top Bottom