Cisco vs Oracle kozi ipi nzuri katika soko la ajira?

Blessed Son

Member
Joined
Apr 23, 2015
Posts
34
Reaction score
23
Naomba ushauri wadau nina mpango wa kusoma mojawapo kati ya hizo kozi, ni ipi kozi nzuri katika soko la ajira?

Natanguliza shukrani!
 
Kwa cisco unaweza piga CCNA na CCNP bado ukapigwa benchi...kwa ushauri piga CCIE Kama unaweza...Kwa Oracle fanya OCP ajira nje nje...
 
Kwa cisco unaweza piga CCNA na CCNP bado ukapigwa benchi...kwa ushauri piga CCIE Kama unaweza...Kwa Oracle fanya OCP ajira nje nje...

Samahani mheshimiwa, unaongea kutokana na uzoefu au maneno uliyoskia kwa watu??
 
Samahani mheshimiwa, unaongea kutokana na uzoefu au maneno uliyoskia kwa watu??

Mimi ni ICT Expert wa mda mrefu kampuni yetu kipindi cha nyuma tulikua tunaajiri CCNP holder na OCA...lakini kwa kipindi hiki hata ukiwa na CCNP au OCA unaweza tusikupe kazi kutokana na wanaoomba kazi wenye CCNP na OCA wapo wengi.

Kwa hiyo tunashauri kama una CCIE au OCP au MCSE ni PM kazi zipo....Gross tunatoa 2.5M kama mzoefu...ila kama unaanza Gross tutakupa 1.8M siyo zaidi ya hapo...kila mwaka huwa tunapandisha mishahara kutegemea na uwezo kazini after Job Performance Review.
 
Kwa cisco unaweza piga CCNA na CCNP bado ukapigwa benchi...kwa ushauri piga CCIE Kama unaweza...Kwa Oracle fanya OCP ajira nje nje...

Sidhani kama unaweza kuruka kwenye CCIE bila kupitia level za Associate na Professional, ni wazo zuri ila mpaka kuifikia hiyo CCIE lazima apige kwanza certificate za chini yake
 
sidhani kama unaweza kuruka kwenye CCIE bila kupitia level za Associate na Professional, ni wazo zuri ila mpaka kuifikia hiyo CCIE lazima apige kwanza certificate za chini yake

CCIE haina prerequisites, mtu yoyote anaweza fanya. Ila inahitaji uzoefu mkubwa sana katika maswala ya networking, unafanya Written exam ukipass unafanya Lab ambayo ni 6 hours exam (Cisco Labs Only-kwa africa hakuna centre kwa sasa). Pia ndo mtihani pekee wa cisco ambao hauna prerequisite.
 
Nashukuru kwa maelezo yako mheshimiwa
 
Duh! Mpo Juu..
 
Hivi kuna CCIE ngapi Tanzania hii?
 
Mkuu samahani hizo couse ni hadi usome kwanza IT?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…