Citizen TV ya Kenya imeripoti Rais Samia kawaachia wafungwa 23 wa kisiasa. Ni akina nani wafungwa wa kisiasa?

Citizen TV ya Kenya imeripoti Rais Samia kawaachia wafungwa 23 wa kisiasa. Ni akina nani wafungwa wa kisiasa?

Hii ni baada ya Upande wa Mashitaka kushindwa kuleta mashahidi mbele ya Hakimu Huruma Shaidi kwa ajili ya usikilizaji wa kesi hiyo leo tarehe 5 May 2021 .

Walioachiwa huru ni Watu 27 akiwemo Halima Mdee , ambaye ni Mbunge asiye na Chama chochote , wote hawa walishitakiwa kwa kosa la kufanya mkusanyiko usio halali na kutotii amri halali katika geti la gereza la Segerea , Jambo lililotafsiriwa kama nia ovu ya kutaka kuvunja Gereza
Walikuwa wafungwa? unaelewa maana ya prisoner?
 
Televisheni ya Citizen ya Kenya imeripoti kuwa Mama Samia ametoa maelekezo wafungwa 23 wa kisiasa waachiwe huru.

Je, Tanzania tuna wafungwa wa kisiasa?

Ni kina nani hao wafungwa wa kisiasa anaowazungumzia Mama Samia?

Au Citizen wanamchafua rais wetu?

Hivi Samia kawa Rais wa Kenya siku hizi? Halafu siku si nyingi Samia atauvaa mkenge wa kuruhusu Wakenya kuingia Bongo bila viza na kufanya kazi bila vibali, hapo ndo tutawajua Wakenya
 
Mdude kakutwa na unga ndani kesi yake sio ya kisiasa.

Lakini je Mdude kaachiwa?
Acha ujinga......ni mahakama gani imethibitisha kua mdude kakutwa na unga?
Kama ni kweli kakutwa na unga, kwa nini mahakama haijamtia hatiani hadi leo hii?,
Kama washitaki wanashindwa kupeleka ushahidi,unategema kesi ni halali hapo?
 
Teh teh teh! Acha nicheke kidhungu mie. Ngoja muwajue vizuri wakenya huenda mlikuwa hamuwajui vizuri. Ila nadhani huyu atakuwa babu seya na wanawe make wale ndo walipigwa lock down ya kisiasa kweli kweli
 
Hii ni baada ya Upande wa Mashitaka kushindwa kuleta mashahidi mbele ya Hakimu Huruma Shaidi kwa ajili ya usikilizaji wa kesi hiyo leo tarehe 5 May 2021 .

Walioachiwa huru ni Watu 27 akiwemo Halima Mdee , ambaye ni Mbunge asiye na Chama chochote , wote hawa walishitakiwa kwa kosa la kufanya mkusanyiko usio halali na kutotii amri halali katika geti la gereza la Segerea , Jambo lililotafsiriwa kama nia ovu ya kutaka kuvunja Gereza
Hao walikuwa wafungwa?
 
Huu ndio ujanja wa kishamba unaokera baadhi yetu. You expect this nonsense from ignorant people not a national media outlet.

Ni sawa na kumsaidia mjinga ambae anaamini mjanja kweli halafu kazungukwa na wajinga wenzake ambao kwenye circle yao hawana utamaduni wa kusaidiana.

Mtu kama huyo siku akikujia na shida zake na kweli anazo ukampa msaada kwenye kichwa chake anaanza kujiona zinga moja la trickster kwa sababu hana mazoea ya kusaidiwa, pengine na yeye mwenyewe hana mazoea ya kusaidia wenzake (au demu ambae ajazoea kupewa hela bila kuombwa ngono, siku ukimsaidia). Watu kama hao wanakuwaga na mawazo fulani ya kifala kweli.

Ndio kama wakenya mama kuonyesha goodwill gesture ili kudumisha community wanaanza kumuona kama zoba fulani hivi wakumpamba kishamba.

Kenyans are so ignorant in their majority.
 
Tanzania ilikuwa imefikia pabaya,walinyimwa uhuru wa kusema, kukusanyika kufanya siasa, kuzushiwa kesi za ajabu na walifungwa waliteswa na kudhalilishwa pia mali zao na akaunti benki fedha kuzuiliwa , uchafuzi wa chaguzi n.k
5 May 2021

HALIMA MDEE NA WENZAKE WAFUTIWA KESI KISUTU, ILE YA KUVUNJA GETI LA SEGEREA "NINA WAACHIA HURU WOTE"





Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imewaachia huru viongozi na wafuasi 27 wa CHADEMA waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya kufanya mkusanyiko na kuvunja geti la gereza la Segerea. Kesi hiyo imefutwa leo Mei 5, 2021 na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya Upande wa Mashtaka kushindwa kupeleka mashahidi mahakamani. Kesi hiyo iliitwa leo kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa lakini Upande wa Mashtaka ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mkunde Mshanga akisaidiana na Wakili wa Serikali, Ester Martin kudai mahakamani hapo kuwa kuwa kwa leo hawana shaidi hivyo wameiomba mahakama kuipangia kesi hiyo tarehe nyingine ya kusikilizwa. Upande wa utetezi ukiongozwa na Wakili Peter Kibatala na Edson Kilatu walipinga kuahirishwa kwa kesi hiyo na kuiomba mahakama kuifuta kwa kuwa upande wa mashtaka wameshindwa kuleta mashahidi kwa muda mrefu. Katika uamuzi wake Hakimu Shaidi amesema; "Kesi hii imeshakuwa na maahirisho kwa muda mrefu hivyo ninawaachia huru washtakiwa wote chini ya kifungu cha 225(5)". Hata hivyo kifungo hicho kinawapa mamlaka jeshi la polisi kuwakamata tena washtakiwa pale wanapokamilisha ushahidi. Walioachiwa ni Wabunge Halima Mdee(41), Ester Bulaya(40) na Jesca Kishoa( 36). Boniface Jacob, Patrick Assenga, Henry Kilewo,Yohana Kaunya,Kedmony Mhembo, Mshewa Karua, Khadija Mwago, Pendo Raphael maarufu kama Mwasomola na mkazi wa Bonyokwa, Cesilia Michael, Happy Abdalla; Stephen Kitomali na Paul Makali, Edgar Adelinj na Reginald Masawe Washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka saba yakiwemo ya kutoa lugha ya kuudhi kuharibu Mali; kufanya mkusanyiko usio kuwa wa halali na kutokutii amri halali iliyowekwa na Jeshi la Magereza na shambulio. Inadaiwa, Machi 13, 2020 , eneo la gereza la Segerea, lililopo wilaya ya Ilala, kwa makusudi washtakiwa walikaidi amri halali ya kuondoka eneo la gereza kwa amani ili eneo hilo libaki wazi, amri hiyo iliyotolewa na askari mwenye namba B 3648, Sajenti John ambaye ni mlinzi wa Geti la gereza hilo. Katika shtaka pili ambalo ni la kufanya mkusanyiko, washtakiwa wanadaiwa kukusanyika isivyo halali kwenye geti la Gereza la Segerea na kusababisha hofu iliyokuwa inapelekea uvunjifu wa amani na utulivu. Pia washtakiwa hao wanadaiwa kuharibu geti kuu la kuingilia na kutokea katika gereza la Segerea mali ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanznia huku Mdee, Bulaya na Jacob wakidaiwa kutoa lugha ya matusi kwa askari Magereza mwenye namba B 3648, Sajent John.
 
Ila Samia atakua ameletwa na Mungu maana yule mjumbe wa kifo alikuwa anatupeleka kubaya
 
Magaidi waliokamatwa dunia nzima na Marekani walikaa mahabusu kule Quantanamol kwa muda wa zaidi ya miaka kumi bila hata kufikishwa mahakamani. Afadhali hawa wa TZ walishafikishwa hata mahakamani mkuu.
Hao ni raia wa nchi zingine wanafanyiwa hivyo na Marekani. Hakuna raia yeyote wa Marekani anafanyiwa hivyo ndani ya nchi yake lakani hapa kwetu ni watanzania wanafanyiwa hivyo ndani ya nchi yao. Huoni huo utofauti?
 
Hivi Samia kawa Rais wa Kenya siku hizi? Halafu siku si nyingi Samia atauvaa mkenge wa kuruhusu Wakenya kuingia Bongo bila viza na kufanya kazi bila vibali, hapo ndo tutawajua Wakenya
Sitaki hata kuyafikiria mkuu, ujambazi wa Munguki utahamia Tanzania,uporaji ndani ya mabenki - who knows hata elements zinazo endelea huko Somalia zinaweza kuwa grafted hapa kwetu kiaina ili Tanzania ionekane mbele ya Kimataifa kwamba hatuna amani - narudia kukumbusha watanzania wenzetu kwamba hata siku moja Wakenya hawatakaa chini kuitakia mema Tanzania - tuishi karibu nao kwa uangarifu sana - tusijifanye ya 1977 does not count at all - hicho ni kipimo tosha cha kupima UTU wao,walitudharirisha sana.
 
3 May 2021
Bukoba, Tanzania

ALIYEKUWA MGOMBEA UBUNGE CHADEMA NA WENZAKE 6 WAACHIWA HURU "HALI YANGU SIO NZURI"



Mahakama ya Hakimu Mkazi Bukoba imewaachia huru washitakiwa saba akiwemo aliyekuwa mgombea wa ubunge kupitia tiketi ya Chadema Jimbo la Bukoba Mjini 2020 Chief Kalumuna ambao walikuwa wanatuhumiwa kwa makosa nane yakiwemo ya kusababisha fujo,kutotii,kusababisha uharibifu wa mali siku ya kuwaapisha mawakala na wagombea tarehe 21 mwezi wa 10 mwaka 2020.

Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Bukoba Joseph Lwambano amesema kuwa ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka haukuthibitishwa hivyo inaonyesha washitakiwa hawakuhusika.

Akiongea nje ya mahakama mshitakiwa namba moja Chief Kalumuna ameeleza furaha yake baada ya kuachiwa huru.

Tarehe 13 May 2021 chief Kalumuna atarudi tena kusimama mahakamani kwa tuhuma ya mambo yaliyotokea tarehe 28 October 2020. Hivyo awaomba wote kumuombea siku hiyo ya kesi nyingine inayomkabili.

Source : millard ayo

N.B

Kutoka Maktaba Uchaguzi wa 2020

 
Mungu mkubwa! Tanzania 2021 yaanza ukurusa mpya. Habari njema hii kwa serikali ya awamu ya sita kujenga taifa lenye umoja ambapo raia wake wanaanza kulindwa wasinyanyaswe haki zao za kiraia na kuishi

Toka maktaba
2020

 
Kwa hiyo Tanzania haikuwai kuwa na wahujumu uchumi zile kelele miaka yote zilikuwa ni za kisiasa?
Uhujumu uchumi ulikuwepo na bado, upo kwa sababu awamu ya 5 haikuutafutia dawa, bali ilitumia kesi hizo kukomowa watu fulani na kukusanya mapato! Wao wenyewe walikuwa wahujumu uchumi, na hawajapona dhambi hiyo, mpaka sasa!
Nje ya mada, lakini ni kwa sababu ya swali lako!
 
Kwa hiyo Tanzania haikuwai kuwa na wahujumu uchumi zile kelele miaka yote zilikuwa ni za kisiasa?
Siasa ya Ujamaa ilikuja kugeuza watu wote wenye fedha kuwa Wahujumu Uchumi

Mimi nakumbuka jamaa yangu alikuwa na kamgahawa kadogo alikamatwa na gunia moja la kilo mia la unga wa Ngano akawekwa kizuizini gerezani huko Bariadi
 
Back
Top Bottom