Civil Engineer/Technician

Sirleh94

Member
Joined
Nov 22, 2018
Posts
12
Reaction score
9
Habari!! Naitwa Salehe nipo Dar, ni muhitimu wa Bachelor of Engineering in Civil kutoka DIT (2024).
Nina uzoefu wa zaidi ya miaka miwili kama Civil Technician (Kuanzia 2018). Pia nimefanya kazi viwandani hivyo kuhusu usalama kazini najua.
Natafuta nafasi ya kazi kama Civil Engineer/Technician. Napokea pia ushauri... Karibuni!!
 

Attachments

Hongera kwa kupata Degree yako Kijana. Zaidi naomba nikushauri yafuatayo kuhusu CV yako:
  1. Ondoa maneno yafuatayo Location na Place of Domicile; Isomeke Nationality
  2. ACADEMIC QUALIFICATIONS: Qualifications zako ziandike kwa kutumia Table au kwa Kiswahili wanasema ni Bango Kitita. Kwa sababu inakuwa rahisi kwa msomaji wa CV yako kupitia kwa haraka na kutokuwa bored na cv yako.
  3. WORK EXPERIENCE: THE SAME AS (2) ABOVE
  4. TRAINING: Orodhesha kozi fupi (Short Courses) ulizowahi kushiriki ambazo zina uhusiano wa moja kwa moja na Profession yako, kwa kuwa zitaongeza strength yako kwa msomaji wa CV yako. Kama hujawahi kushiriki katika short course yoyote related to your profession ni vizuri usiliandike eneo la Training.
  5. TECHNICAL SKILLS: Naziona kama ni sehemu ya ulichojifunza ulipokuwa Chuoni DIT hivyo nakushauri uondoe. Maana msomaji wa CV yako anaweza kukuona huna ufahamu wa Profession yako.
  6. INTERESTS: Andika HOBBIES Badala ya Interests. Vilevile, usirudie kuandika masuala yanayohusu Profession yako kwenye HOBBIES e.g Structural Design and Analysis. Mfano wa HOBBIES ni kama; Reading Books, Watching TV, Travelling etc
  7. CAREER OBJECTIVE: Herufi O haipo
  8. REFERREES: Ondoa Jina la Kwanza maana linaonesha kuwa ni Jina la Ndugu yako. Weka Jina la Lecturer aliyekufundisha hapo DIT na hakikisha anakufahamu vizuri, kama hakufahamu vizuri ongea naye ili akiulizwa aweze kukuelezea vizuri ulivyo. Ongezea Jina la Mtu mwingine mwenye Title Serikalini au hata Mashirika Binafsi yenye Profile kubwa.
  9. Mwisho: Haya ni maoni tu. Hivyo yasichukuliwe kuwa ndio Msahafu wa Uandishi wa CV.
 
Nashukuru kwa ushauri wako🙏 Nimeupokea!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…